Data za zaidi ya wateja 120 wa benki kuu ya Thailand zadukuliwa

Data za wateja wa benki kuu ya Thailand (BOT) zimedukuliwa katika matawi mawili makubwa ya kibiashara.

Data za zaidi ya wateja 120 wa benki kuu ya Thailand zadukuliwa

Data za wateja wa benki kuu ya Thailand (BOT) zimedukuliwa katika matawi mawili makubwa ya kibiashara.

Kulingana na shirika la habari la Sinhua,benki za "Kasikorn bank" na "Krung Thai Bank" zimethibitisha kuwa data za wateja zaidi ya 120 zimeibiwa.

Wakati wataalam wa usalama wa BOT wameahidi kuongeza hatua za usalama, watendaji wa benki zote wamedai kuwa hawakuona dalili zozote za wizi wakati data hizo zikidukuliwa.

Kiongozi wa "Krung Thai Bank", Payong Srivanich amesema kuwa wezi hao wametumia mbinu za kisasa kupata taarifa zote za maelfu ya wateja na kisha kutumia taarifa hizo kuomba mikopo kupitia mtandao.

Kiongozi wa benki ya Kasikorn ,Pipit Aneaknithi amesema kuwa wadukuzi hao  wamechukua data za maelfu ya wateja kwa kutumia huduma ya dhamana ya benki mtandaoni.

 Habari Zinazohusiana