EU,Urusi na Ukraine kuendeleza mazungumzo kuhusu gesi

Umoja wa Ulaya,Urusi na Ukraine zimekubaliana kuendeleza mazungumzo kuhusu gesi.

EU,Urusi na Ukraine kuendeleza mazungumzo kuhusu gesi

Umoja wa Ulaya,Urusi na Ukraine zimekubaliana kuendeleza mazungumzo kuhusu gesi.

Nchi hizo zimekubaliana kuendelea na amzungumzo kuhusu usafirishaji wa gesi kutoka Urusi kuelekea Umoja wa Ulaya kwa kupitia Ukraine.

Makamu wa rais wa Umoja wa Ulaya Maros Sefcovic amesema kuwa amefanya mazungumzo ya kina na waziri wa nishati wa Urusi  Alexander Novak na waziri wa mambo ya nje wa Ukraine Pavlo Klimkin.

Kutakuwa na mkutano mwingine kati ya nchi hizo ifikapo mwezi Oktoba.

Umoja wa Ulaya unatumaini kufanya makubaliano na Urusi na Ukraine ili kuweza kupata gesi kutoka Urusi kupitia Ukraine.

Mkataba wa gesi kati ya Ukraine na Urusi unatarajia kuisha wakati wake ifikapo 31 Desemba 2019.Habari Zinazohusiana