Msaada kwa wapalestina kutoka kwa Maradona

Nyota wa kabumbu wa zamani Diego Maradona  kutoa msaada  kwa wapaletina

Msaada kwa wapalestina kutoka kwa Maradona

 

Nyota wa zamani wa kabumbu wa kimataifa ambae hajapata mapinzani  Diego Maradona  amekutana na raia wa mamlaka ya wapalestina Mahmoud Abbas katika michuano ya kombe la dunia iliokuwa ikiendelea  nchini Urusi.

Katika mazungumzo yao nyota huyo wa kabumbu amesema  kuwa  yupo  pamoja na wapalestina  na yeye anjisikia kama miongoni mwao katika nafsi yake.

Maradona ameonekana akiwa na Mahmoud Abbas katika picha zilizosambazwa katika mitandoa ya kijamii. Maradona katika ukurasa wake wa Instagram amesema kuwa Abbas anahitaji amani, ni mtu wa amani na ana haki yakutekeleza jambo hilo.

Nyota huyo kutoka Argentina alikwisha onesha msimamo wake kuhusu mzozo wa Mashariki ya Kati   mwaka 2012 kwa kusema kuwa ana heshima kubwa kwa wapalestina na ana waonga mkono. Maradona pia alizungumza  wakati wa vita kati ya Israel na Hamas mwaka 2014 na kuikemea Israel.

 Habari Zinazohusiana