Watoto wa Palestina wauawa katika shambulizi la Israel

Watoto wawili wa kipalestina wameuawa katika shambulizi la anga lililofanywa na jeshi la Israel katika ukanda wa Gaza.

Watoto wa Palestina wauawa katika shambulizi la Israel

Watoto wawili wa kipalestina wameuawa katika shambulizi la anga lililofanywa na jeshi la Israel katika ukanda wa Gaza.

Kwa mujibu wa habari,shambulizi hilo lilikuwa limefanywa likilenga jengo la al-Katiba ambalo bado linafanyiwa ujenzi.

Kati ya waliopoteza maisha mtoto mmoja alikuwa na umri wa miaka 15 na mwingine 14.

Watoto wengine 14 wameripotiwa kujeruhiwa.

Kulingana na jeshi la Israel,roketi 91 zilirushwa kutoka Gaza kuelekea upande wao.Habari Zinazohusiana