Wizara ya kilimo ya Palestina yapiga marufuku kuingizwa kwa matunda Gaza kutoka Israel

Wizara ya kilimo ya mamlaka ya wapalestina yapiga marufuku kuingizwa kwa matunda Ukanda wa Gaza kutoka Israel

Wizara ya kilimo ya Palestina yapiga marufuku kuingizwa kwa matunda Gaza kutoka Israel

Wizara ya kilimo ya  mamlaka ya wapalestina  yapiga marufuku  Jumatano kuingia matunda Ukanda wa Gaza kutoka Israel kupitia katika kituo cha mpakani cha Karam Abu Slem Kusini.

Uamuzi huo umechukuliwa  baada ya Israel  kupiga marufuku mboga mboga kutoka Ukanda wa Gaza kuingia Israel.

Mkurugenzi wa masuala ya biashara mipakani mwa maeneo ya wapalestina amefahamisha kuptia kituo cha habari cha Anadolu kuwa uamuzi huo ni  jibu kwa  kuwekea vikwazo bidhaa kutoka katika Ukanda wa Gaza.

Ukanda wa Gaza ulikuwa ukinunua zaidi ya tani 20 za matunda Karam Abu Salem kabla ya kuchukuliwa kwa uamuzi huo .

Zaidi ya tani  200 za mboga mboga kutoka Ukanda wa Gaza zilikuwa zikiingia Israel.

 Habari Zinazohusiana