Historia ya wavuta sigara Marekani

Utafiti umeonyesha kuwa kiwango cha wavuta sigara nchini Marekani kimefikia hatua yake ya chini tangu takwimu za kwanza zilitolewa mwaka wa 1965

Historia ya wavuta sigara Marekani

Utafiti umeonyesha kuwa kiwango cha wavuta sigara nchini Marekani kimefikia hatua yake ya chini tangu takwimu za kwanza zilitolewa mwaka wa 1965.

Asilimia 13.9 tu ya watu wazima wa Marekani walivuta sigara mwaka 2017, chini ya asilimia 16 mwaka 2016 na asilimia 20.8 mwaka 2006.

Utafiti ulikusanywa na wanasayansi katika Kituo cha Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa (CDC).

Katikati ya miaka ya 1960, asilimia 42 ya watu wazima walivuta sigara.

Hata hivyo, takwimu zinaonyesha kuwa Wamarekani zaidi ya milioni 30 wanaendelea kuvuta.

Inaonekana kuwa kuna tofauti fulani kutoka mahali hadi mahali katika suala la idadi ya watu wanaovuta sigara.

Katika maeneo ya vijijini, zaidi ya asilimia 21 ya watu wazima wanavuta sigara ikilinganishwa na asilimia 11 ya wale wanaoishi mijini.Habari Zinazohusiana