Uturuki na azimio la Umoja wa Mataifa kuhusu Palestina

Uturuki yazungumzia azimio la Umoja wa Mataifa kuhusu wapalestina na kulindiwa usalama

Uturuki na azimio la  Umoja wa Mataifa kuhusu Palestina

 Rais wa Uturuki Recep Tayyıp Erdoğan asema kuwa kupitishwa kwa azimio ambalo linalenga wapalestina kulindiwa usalama bila shaka  ni jambo ambalo limekera na kupokelewa kinyume na Marekani.

Baraza la Umoja wa Mataifa  limepitisha msuada ambao lengo lake ni kuwalindia usalama wapalestina.

Kwa mujibu wa msamaji wa serikali na ikulu ya rais Ankara Ibrahim Kalın,  atua hiyo iliopigwa Umoja wa Mataifa ni  ushindi mkubwa.

Ibrahim Kalın ameendelea kusema kuwa Uturuki  itaendelea kuwa bega kwa bega kupigania na kutetea haki za wapalestina.

Waziri wa mambo ya nje wa Uturuki Mevlüt Çavuşoğlu pia amezungumzia kuhusu suala hilo kwa kusema kuwa jumuiya ya kimataifa  kwa mara nyingine imeonesha kuwa wapalestina  hawatoachwa katika madhila yanayowakibili kwa kudhulumiwa.Habari Zinazohusiana