Ombi la kuwalinda wapalestina lapitishwa na Umoja wa Mataifa

Ombi la kuwalindia usalama wapalestina lapitishwa na baraza la Umoja wa Mataifa

Ombi la  kuwalinda wapalestina lapitishwa na Umoja wa Mataifa

Baraza la Umoja wa Mataifa  lapitisha ombi la  kulindiwa usalama wapalestina.   Baraza la Umoja wa Mtaifa limekutana katika mkutano maalumu kuzungumzia  ombi kuhusu   kulindiwa usalama.

Ombi hilo limewakilishwa Umoja wa Mataifa kwa juhudi kubwa ya Uturuki  ikiungwa mkono na Algeria. Ombi hilo la kuwalindia usalama wapalestina limetishwa na  na baraza la Umoja wa Mataifa wakati ambapo Marekani ikitumia kura yake ya turufu. 

Msuada huo kuhusu wapalestina kulindiwa usalama umepitishwa na mataifa 120 wanachama wa Umoja wa Mataifa.

 Mataifa 45  hayakuonesha msimamo kuhusu pendekezo hilo,  mataifa kama Marekani, Israel, Australia, visiwa vya Marshall, Nauru, Togo, visiwa vya Salomon na Micronezia  yamepinga msauda na pendekezo hilo.

Kwa upande  mwingine, pendekezo la Marekani kukemea  chama cha Hamas  limetupiliwa mbali.

Mahmud Abbas kiongozi wa mamlaka ya wapalestina amepongeza atua hiyo kwa kusema kuwa ni ushindi wa haki na sheria ya kimataifa.

Vile vile Umoja wa Mataifa umetolea wito Israel  kuacha kutumia nguvu zaidi dhidi ya wapalestina na kuondoa  vikwazo  vinavyolikabili eneo la Ukanda wa Gaza.

 

 

 Habari Zinazohusiana