Papa Francis asikitishwa na mauaji Ukanda wa Gaza

Kiongozi wa kanisa Katoliki ulimwenguni Papa Francis asikitishwa na mauaji yalifanyika Ukanda wa Gaza

Papa Francis asikitishwa na mauaji Ukanda wa Gaza

Kiongozi wa kanisa katoliki ulimwenguni Papa Francis  afahamisha kusikitishwa na mauaji ya Ukanda wa Gaza na kutoa wito wa mazungumzo bain aya Palestina na Israel.

Papa Francis ametoa wito wa kusitisha ghasia na mauaji katika mji mtakataifa ambao ni kitovu cha imani ulimwenguni.

Kiongozi wa kanisa katoliki ulimwenguni ameyazungumza hayo  Jumatatu  akiashiria wapalestina waliouawa na jeshi la Israel katika maandamano ya amani Ukanda wa Gaza. Jeshi la Israel lilitumia  risasi za moto kuwatawanya waandamanaji na kusababisha maafa.

Taarifa kuhusu  amani na utulivu katika ardh takatifu ilitolewa na  tovuti ya « Vatican News »  Jumatano.Habari Zinazohusiana