Erdoğan : "Tunakabiliana na ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu"

Rais Erdoğan asema kuwa makabiliano na ukiukwaji wa haki za binadamu katika maeneo ya wapalestina ni mkubwa

Erdoğan : "Tunakabiliana na ukiukwaji mkubwa wa haki za  binadamu"

Rais wa Uturuki Recep Tayyıp Erdoğan asema kuwa   Palestina kuna ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu akizungumzia ugaidi wa Israel na mauaji yalifanywa Ukanda wa Gaza katika  maandamano.

Rais amechagia chakula cha "Iftar" , mlo maalumu ambao haundaliwa jiano  kwa waislamu waliodiriki  ibada ya funga uliotaarishwa ikulu . Katika mlo huo ndugu jamaa wa wahanga na mashujaa  wanaojitolea kwa ajili ya Uturuki.  Rais Erdoğan amesema kuwa ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu unashuhudiwa Palestina, na kosa kubwa kwa wapalestina kutetea ardhi . Watu zaidi 60 wameuawa na jeshi la Israel  huku wengine  zaidi ya 3 000 wamejeruhiwa.

Watu hao waliuawa na kujeruhiwa wakiwa katika maandamano ya kupinga ufunguzi wa ubalozi wa Marekani mjini Yerusalemu na kupinga pia kuzuiliwa kwa wapalestina kurejea katika makaazi yao.

Marekani ilifunguwa ubalozi wake mjini Yerusalemu Jumatatu bila ya kujali maazimio ya kimatafa na makubaliano ya kimataifa  kuhusu Yerusalemu.

Rais Erdoğan amesema kuwa kamwe Uturuki haitofumbia macho mauaji na ukiukwaji wa haki za binadamu unaondelea katika maeneo ya wapalestina.

Rais Erdoğan amezungumzia udhaifu wa jumuiya ya kimataifa kuzuia mauaji katika maeneo tofauti kama Boznia, Barani Afrika, Somalia, Irak , Syria na meneo mengine. Kufumbia macho mauaji ya Palestina jumuiya ya kimataifa inajichimbia kaburi lake.

 

 Habari Zinazohusiana