Waziri mkuu wa Uturuki asema kuwa UM waonesha udhaifa usiokuwa na mfano

Waziri mkuu wa Uturuki Binali Yıldırım azungumzia udhaifu wa Umoja wa Mataifa kuhusu mauaji ya wapalestina na jeshi la Israel

Waziri mkuu wa Uturuki asema kuwa UM waonesha udhaifa usiokuwa na mfano

Waziri mkuu wa Uturuki Binali Yıldırım asema kuwa  Umoja wa Mataifa  umeonesha udhaifu usiokuwa na kifani kufuatia mauaji ya wapalestina Ukanda wa Gaza na jeshi la Israel.

Binali Yıldırım amesema kuwa wapalestina 62 wameuawa na jeshi la Israel katika maandamano ya amani huku Umoja wa Mataifa ukisailia kimya bila ya kutoa tamko lolote lile.

Akizungumza na waandishi wa habari  mjini Ankara Binali Yıldırım amesema kuwa alikuwa na matumaini kuwa Ramdhani itakuwa mwezi wa faraja na Umoja ila jambo la kusikitisha wapalestina wameanza Ramadhani wakiwa katika majonzi huku damu zao zikimwagika.

Kitendo cha Marekani kuhamisha ubalozi wake Yerusalemu, jiji na kitovu cha imani ulimwenguni ni kinyume na makubaliano ya  Umoja wa Mataifa.

 

 

 Habari Zinazohusiana