Kuhani wa kiyahudi mjini London asema kuwa Israel ni taifa hatari ulimwenguni

Kuhani wa jamii ya kşyahudi mjini London apokelewa na rais wa Uturuki Recep Tayyıp Erdoğan  katika ziara yake nchini Uingereza

Kuhani wa kiyahudi mjini London asema kuwa Israel ni taifa hatari ulimwenguni

Rais wa Uturuki Recep Tayyıp Erdoğan amempokea kuhani wa jamii na imani ya kiyahudi mjini London katika ziara yake nchini Uingereza. Kwa mujibu wa  kuhani huyo na tume alioshirikiana nayo amesema kuwa  taifa la Israel ni taifa hatari mno ulimwenguni.

Kuhani na kiongozi wa jamii ya kiyahudi mjini London Elahanan Beck  alipokewa na rais Erdoğan katika hafla maalumu ilioandaliwa.

Kuhani huyo baada ya kuzungumza na rais wa Uturuki alifanya mahojiano na waandishi wa habari na kuwafahamisha kuwa kuwasaidia wazayuni sio kuwasaidia  wayahudi, iwapo mtataka kuwasaidia wayahudi basi fanyeni  kama anavyofanya  rais wa Uturuki. Beck aliendelea kuzungumza na waandishi wa habari akiwalenga viongozi wa Marekani na Uingerea  akisema kuwa kuisaidia Israel  sio kusaidi  jamii ya wayahudi.

Kuwasaidi wayahudi  ni kusimama imara na kuonesha msimamo thabiti dhidi ya taifa la Israel, dhidi ya taifa ambalo linakalia kimabavu ardhi ya wapalestina. Kuhuan Beck amesema kuwa wayahudi na wapalestina  wanaweza kuishi kwa amani na waislamu.

 Habari Zinazohusiana