Ngome kubwa ya magaidi yagu duliwa Afrin Syria

Ngome kubwa ambayo imekuwa ikitumika kuwahifadhi magaidi katika eneo la Afrin imepatikana

Ngome kubwa ya magaidi yagu duliwa Afrin Syria

Ngome kubwa ambayo imekuwa ikitumika kuwahifadhi magaidi katika eneo la Afrin imepatikana.

Kwa mujibu wa habari,ngome hiyo ya chini ya ardhi imepatikana na ina uwezo wa kuhifadhi magaidi takriban 1000.

Ngome hiyo imepatikana pale wanajeshi wa Uturuki pamoja na wale wa jeshi huru la Syria walipokuwa wakisafisha maeneo mbalimbali baada ya kulikomboa jimbo la Afrin.

Baada ya ugunduzi huo imeonekana kuwa ilikuwa ni vigumu kujua kama kuna ngome kubwa kama hiyo kutokana na kufunikwa kwake na miti.

Jeshi la Uturuki limefanikiwa kuikomboa Afrin kutoka katika mikono ya magaidi.

Operesheni ya tawi la mzaituni iliyoanzishwa 20 Januari imeonyesha mafanikio.


Tagi: magaidi , ngome , Afrin

Habari Zinazohusiana