India yaandamana kupinga mauaji ya binti wa miaka minane

Kumekuwa na maandamano katika miji tofauti kupinga mauji na ubakaji wanaotendewa mabinti mdogo nchini India

India yaandamana kupinga mauaji ya binti wa miaka minane

Kumekuwa na maandamano katika miji tofauti kupinga mauji na ubakaji wa binti mdogo wa miaka nane nchini India.

Maandamano hayo yameonekana katika miji tofauti kama vile New Delhi, Mumbai, Chandigarh, Bengaluru, Bhopal, Indore, Ajmer, Surat, Goa, Thiruvananthapuram na mingine mingi.

Mnamo Januari,binti mdogo wa miaka nane alitekwa katika eneo la Kathua.

Baada ya siku kumi mwili wa mtoto huyo ulikuwa umetelekezwa msituni.

Uchunguzi umeonyesha mtoto huyo alitekwa,kuteswa,kubakwa zaidi ya mara moja na kisha kuuawa.

Hayo yote yalifanyika ndani ya moja ya hekalu Hiranagar.

Ripoti zimeonyesha kuwa binti huyo alibakwa na kundi la wahindu wakiwemo maafisa polisi.

Mawaziri wawili walioonyesha dalili za kutetea washutumiwa hao wamelazimika kujiuzulu kutokana na hasira  ya wananchi nchini India.Habari Zinazohusiana