Umoja wa Ulaya wamtaka Assad kuacha mashambulizi Ghuta

Umoja wa Ulaya umemtaka Assad kusitisha mashambulizi yake mashariki mwa Ghuta

Umoja wa Ulaya wamtaka Assad kuacha mashambulizi Ghuta

Umoja wa Ulaya umemtaka Assad kusitisha mashambulizi yake mashariki mwa Ghuta.

Federica Mogherini akizungumza katika bunge la Umoja wa Ulaya amesema kuwa pendekezo la Urusi la kuwa mapigano yawe yanasitishwa kwa muda fulani ili mahitaji ya binadamu yaweze kusambazwa kwa raia ni  hatua muhimu lakini haitoshi kuyasitisha mashambulizi hayo.

Mogherini ameongeza kwa kusema kuwa jeshi la Assad limekuwa likiendelea kuwashambulia raia huku huduma za afya zikiangamizwa  na raia wanaojaribu kukimbia wakimiminiwa risasi.

Kwa mujibu wa habari,mnamo mwezi Aprili kutakuwa na mkutano Brussels kujadili kusitishwa kwa mapigano mashariki mwa Ghuta.

Kwa miezi minane jeshi la Assad limekuwa likiizingira Ghuta Mashariki hali inayosababisha kuwa vigumu kwa huduma za kibinadamu kufika katika eneo hilo ikiwemo chakula.Habari Zinazohusiana