Korea Kaskazini haijazungumza lolote toka Trump akubali kukutana na Kim

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Rex Tillerson amesema kuwa Korea Kaskazini imekaa kimya toka Trump akubali kukutana na Kim Jong Un.

Hayo Tillerson ameyazungumza wakati alipofanya mkutano na waandishi wa habari katika mji mkuu wa Abuja nchini Nigeria.

Tillerson amesisitiza kuwa Marekani inasubiria kauli ya moja kwa moja kutoka Pyongyang.

Siku chache zilizopta mshauri wa usalama wa taifa wa Korea Kusini Chung Eui-Yiong alitangaza  White House kuwa Kim Jong Un yupo tayari kufanya mazungumzo na Trump.

Tillerson amesema kuwa sehemu ya kufanyika mkutano huo bado haijaandaliwa lakini ni vyema mazungumzo hayo yakafanywa kimya kimya.

Trump na Kim wana historia ya muda mrefu ya kurushiana maneno na Trump hasa alikuwa akimtishia Kim Jong Un na kumuita "Little Rocket Man"

Kim naye alimjibu Trump kwa kumwambia "Mbwa mwenye hofu hubweka kwa nguvu"

Hata hivyo una matumaini kuwa mahusiano kati ya viongozi hao wawili yataimarika baada ya mkutano huo kufanyika.

 Habari Zinazohusiana