Njia mpya ya wahamiaji haramu kuingia barani Ulaya

Wahamiaji haramu watumia Bosnia Herzegovina kuingia Ulaya Magharibi

Njia mpya ya wahamiaji haramu kuingia barani Ulaya

Wahamiaji haramu wagundua njia mpya ya kuingia katika mataifa ya Ulaya Magharibi kwa kupitia nchini Bosnia Herzegovina.

Hapo awali  wahamiaji walikuwa wakipitia nchini Ugiriki, Makedonia, Serbia, Hungary au Kroasia kuingia katika mataifa ya Ulaya Magharibi.

Njia hiyo ambayo ilikuwa ikitumiwa na wakimbizi ilifungwa Machi mwaka 2016.

Kwa sasa wahamiaji haramu na wakimbizi wanajaribu kutumia Kroasia kupitia Bosnia Herzegovina kuingia katika mataifa ya Ulaya Magharibi kutafuta hifadhi.

Katika kipindi hiki cha baridi, maimamu katika hutoa hifadhi za muda kwa wahamiaji wanaoathirika na baridi katika safari zao.

Wahamiaji 35 wamepewa hifadhi  na maimamu mjini Sarayevo wajikinge na baridi.

Wengi miongoni mwa wahamiaji hao ni raia kutoka Pakistan, Afghanistan, Syria, Libya na Morocco.

Jeshi la Polisi Bosnia  limefahamisha kuwa watu zaidi ya 750 wameingia nchini humo kinyume cha sheria  Januari  mwaka 2018 wakştaraji kuendelea na safari yao Ulaya Magharibi.Habari Zinazohusiana