Waziri wa mambo ya nje wa Uholanzi ajiuzulu baada ya kuzungumza uongo kuhusu Putin

Waziri wa mambo ya nje wa Netherlands Halbe Zijlstra amejiuzulu siku moja baada ya kukubali kuwa alidanganya kuhusu rais Vladimir Putin.

Mnamo mwaka 2016,wakati wa mkutano wa chama cha VVD Zijlstra alisema kuwa Putin alisema ana matarajio ya kujenga "Urusi iliyo bora" mwaka 2006.

Alitangaza kujiuzulu kwake katika hotuba yake iliyokuwa imejaa hisia kali wakati wa mkutano wa wakilishi.

Kwa mujibu wa habari,Zijlstra amesema kuwa uongo huo ni kosa lake kubwa katika safari yake ya siasa na kwamba nchi yake inahitaji waziri bora kuliko yeye.

Kujiuzulu kwake kumekuja siku moja kabla ya kupangwa kwa ziara yake mjşni Moscow ambapo alitarajia kukutana na mwenzake Sergey Lavrov.

Tamko la "Urusi iliyo bora" limeimaliza safari ya uwaziri mkuu wa Zijlstra ambayo ilianza Oktoba 2017.

 Habari Zinazohusiana