Rais wa Palestina akutana na Putin mjini Moscow

Rais wa Palestina Mahmoud Abbas amesema kuwa taifa lake halidhani kuwa Marekani ndio nchi pekee inayoweza kusuluhisha mgogoro kati ya Israel na Palestina.

Hayo rais Abbas ameyazungumza katika mkutano na rais wa Urusi Vladimir Putin Moscow.

Abbas amesema Palestina haikubaliani na matendo na uamuzi wa Marekani.

Katika mkutano huo Putin amemwambia rais wa Palestina kuwa kabla ya kufanyika kwa mkutano huo,rais Putin tayari alikuwa ameongea na Trump kuhusu suala zima la Palestina na Israel.

Mzozo ulianza pale Marekani ilipotoa uamuzi wa kuutambua mji wa Jerusalem kama mji mkuu wa Israel.Habari Zinazohusiana