Marekani imetumia kiwango cha dola trilioni 7 kwa ajili ya Mashariki ya Kati

Rais Donald Trump asema kuwa Marekani imetumia kiwango cha dola trilioni 7 kwa ajili ya Mashariki ya Kati

Marekani imetumia kiwango cha dola trilioni 7 kwa ajili ya Mashariki ya Kati

 

Rais wa Marekani Donald Trump amesema kuwa hadi kufikia sasa Marekani imekwishatumia kiwango cha dola trilioni 7 kwa ajili ya Mashariki ya Kati.

Akizungumzia kuhusu mpango wa matumizi ya mwaka 2019 Marekani, Trump amesema kuwa  Marekani inatumia gharama kubwa kwa ajili ya Mashariki ya Kati.

Kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa katika miezi kadhaa ya nyuma, ni kwamba Marekani imetumia kiwango cha dola trilioni 7 kwa ajili ya Mashariki ya Kati pekee.

Trump amesema kuwa  ni kosa kubwa ila hali halisi ndio kama hiyo.

Trump amesema kuwa  Mashariki  ni eneo kwa sasa ambalo lipo katika hali mbaya kuliko ilivyokuwa  miaka 17 iliopita  kabla ya kuanzishwa kwa operesheni ambayo haikuwa na umuhimu wala busara.

Trump alikemea kukaliwa kimabavu kwa Irak na Marekani  katika kampeni zake .Habari Zinazohusiana