Waziri wa mambo ya nje wa Uturuki aitupia lawama Marekani kuhusu kundi la FETÖ

Waziri wa mambo ya nje wa Uturuki Mevlüt Çavuşoğlu aitupia lawama na kuitahadharisha Marekani na kundi la FETÖ

Waziri wa mambo ya nje wa Uturuki aitupia lawama Marekani kuhusu kundi la FETÖ

 

Waziri wa mambo ya nje wa Uturuki Mevlüt Çavuşoğlu katika ziara yake nchini Marekani  amesema kuwa ulimwengu umetambua ni kiasi gani kundi la FETÖ ni kundi lisilostahili kuepo na ipo siku ambayo Marekani inatambua hilo.

Waziri huyo wa mambo ya nje wa Uturuki ameitupia lawama Marekani kutokana na ukaribu wake na kundi hilo.

Waziri wa mambo ya nje wa Uturuki amekutana na raia wa Uturuki waishio Los Angeles  na kufahamisha kuwa mungu akipenda Marekani pia itatambua ni kiasi gani kundi la FETÖ ni kundi hatari.

Licha ya ombi la Uturuki kurejeshwa kwa kiongozi  wa kundi la FETÖ  kukataliwa na kutokuanzishwa kwa uchunguzi Marekani ipo siku itatambua uhatari wa kundi hilo amezidi kusema waziri wa mambo ya nje wa Uturuki.

Waziri Mevlüt Çavuşoğlu amezungumzia pia kuhusu kuyumba kwa ushirikiano na Mrekani kutokana na msaada wa kijeshi kutoka Marekani kwa kundi la kigaidi la PYD ambalo ni tawi la kundi la kigaidi la PKK, tunajaribu kutatua mzozo huo kwa mazungumzo alisema  waziri wa mambo ya nje wa Uturuki.

 Habari Zinazohusiana