Uturuki yalaani shambulizi lililolenga kanisa nchini Pakistan

Uturuki yalaani shambulizi la kşgaidi lililolenga kanisa Quetta nchini Pakistan

Uturuki yalaani shambulizi lililolenga kanisa nchini Pakistan

 

Serikali ya Uturuki yalaani vikali shambulizi la kigaidi lililotekelezwa dhidi ya kanisa Jumapili Quetta nchini Pakistan.

Shambulizi hilo lililsababisha vifo vya watu  wanane na kuwajeruhi wengine zaidi ya 40.

Taarifa zilizotolewa na vyombo vya usalama zimefahamisha kuwa shambulizi hilo lilitekelezwa na watu wawili ambapo mmoja alitoa muhanga huku mwingine aliejaribu kutoroka kuuawa na Polisi kwa kupigwa risasi.

Kundi la wanamgambo wa Daesh limejinasibu kuhusika na shambulizi hilo.

Uturuki kupitia wizara yake ya mambo ya nje imelaani vikali shambulizi hilo na kutoa pole kwa familia za wahanga.Habari Zinazohusiana