Rais wa Palestina kufanya ziara Saudi Arabia

Rais wa Palestina Mahmoud Abbas anatarajia kufanya ziara Riyadh siku ya Jumanne kwa ajili ya kufanya mazungumzo na nfalme Salman bin Abdulaziz na mwana wa mfalme Mohammed bin Salman.

Kwa mujibu wa habari,rais huyo atafanya ziara kwa ajili ya kuzungumza juu ya agenda ya Jerusalem kama mji mkuu wa Palestina.

Hapo awali,vituo vya habari vya Israel vimekuwa vikiandika habari kuwa Saudi Arabia ilimkandamiza rais wa Palestina na kumlazimisha afanye makubaliano na Israel.

Hata hivyo,balozi wa Palestina nchini Saudi Arabia amekanusha madai hayo na kusema kuwa ni propaganda za kutaka kuharibu mahusiano kati ya Saudi Arabia na Palestina.

Desemba 6 rais wa Marekani  Donald Trump alitangaza kuutambua mji wa Jerusalem kama mji mkuu wa Israel.

Hatua hiyo imepingwa na kukemewa na mataifa mengi ya kiislamu na yale yasiyokuwa ya kiislamu.Habari Zinazohusiana