Viongozi wa mataifa ya kiislamu wakutana mjini Istanbul nchini Uturuki

Viongozi wa mataifa ya kiislamu  wakutana mjini Istanbul nchini Uturuki kujadili suala lla Jerusalem

Viongozi wa mataifa ya kiislamu wakutana mjini Istanbul nchini Uturuki

 

Shirikisho la kiislam linakutana katika mkutano wake  ussikuwa wa kawaida  chini ya usimamizi wa Uturuki baada ya uamuzi wa rais wa Marekani Donald Trump kutangaza kuutambua mji wa Jerusalem kama mji mkuu wa Israel.

Mkutano huo ulitolewa wito na Uturuki baada ya Trump kutangaza kuwa ubalozi wake ulioko Tel Aviv utahamia Jerusalem kwa kuwa serikali yake inatambua mji huo kama mji mkuu wa Israel.

Mtaifa 57 yanatarajiwa kushiriki katika mkutano huo.

Viongozi kutoka nchini Afghanistan, Azerbaijan, Bangladesh, Indonesia, Palestina , Guinea, Iran, Qatar, Kuweït, Libya,Lebanon, Somalia, Sudan, Togo, Jordan ,Yemen ,Djibouti, ,Malaisia , Pakistan , Comoro, Oman Kazakistan na Uzbekistan watakuepo.

Rais wa Cyprus Kaskazini na rais wa Venezuela Nicolas Maduro pia watashiriki katika mkutano huo.

 Habari Zinazohusiana