Vladimir Putin kuwania kiti cha urais kwa mara nyingine Urusi

Rais Vladimir Putin atangaza kuwani kiti cha urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2018 Urusi

Vladimir Putin kuwania kiti cha urais kwa mara nyingine Urusi

Rais wa Urusi Vladimir Putin ametangaza kuwa atawania kiti cha urais katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika  nchini humo ifikapo Machi 18 mwaka 2018.

Hayo Putin aliyafahamisha akiwa hafla ilioandaliwa Nijini Urusi.

Rais Putin aliweka wazi uamuzi wake kuwa atashiriki kama mgombea wa kiti cha uraisi katika uchaguzi huo mwaka 2018.

Uchaguzi huo umeonekana kuandaliwa kufanyika siku ambayo kunaadhimishwa eneo la Krime kumilikiwa na Urusi.

Kwa mujibu wa wadadisi wa masuala ya kisiasa Putin anaonekana kuwa atasalia katika kiti cha urais.

Takwimu zinaonesha kuwa asilimia 68 za rarusi watamchagua rais Putin.

 Habari Zinazohusiana