Uamuzi wa Trump wakemewa White House

Viongozi wawili wa ngazi za juu ikulu wakemea uamuzi wa Trump kuhusu jiji la Jerusalem

Uamuzi wa Trump wakemewa White House

 

Baadhi ya viongozi katika ikulu ya White House nchini Marekani wanasema kuwa kitendo cha Trump kutangaza kutambua jiji la Jerusalem kama mjini mkuu wa Israel kutaathiri kwa kiasi kikubwa harakati za kusaka amani ya kudumu  baina ya Israel na Palestina Mashariki ya Kati.

Viongozi wawili wa ngazi ya juu ikulu ya rais mjini Washington ambao hakupendelea majina yao yatajwe  wamekiambia kituo cha habari cha CNN wanasikitishwa na uamuzi ulichukuliwa na Trump kuhusu jiji la Jerusalem kuwa ni mji mkuu wa Israel.

Kwa mujibu wa viongozi hao uamuzi huo utaathiri harakati za kusaka amani.

Viongozi hao wamesema kuwa wanataraji kuwa hali hiyo ya mtafaruku katika kusaka amani isichukuwe muda mrefu bali ipatiwa ufumbuzi.

 Habari Zinazohusiana