Sudan kusitisha ushirikiano wake na Korea Kaskazini

Washington yasema kuwa serikali ya Sudan atasitisha ushirikiano wake wa kibiasha na kijeshi na Korea Kaskazini

Sudan kusitisha ushirikiano wake na Korea Kaskazini

 

Serikali ya Marekani imesema kuwa Sudan itasitisha ushirikiano wa kibiarsha na kijeshi na serikali ya Korea Kaskazini. Taarifa hiyo imetolewa na msemaji wa serikali ya Marekani Heather Naouert kwa waandishi wa habari Ijumaa.

Heather alisema kuwa Sudan itasitisha ushirikiano wake huo na Korea Kaskazini kutokana na vitisho na uhatari ya mpango wa nyuklia wa Korea.

Nauert amesema  uamuzi huo umepongezwa na serikali ambao umechukuliwa wakati wa ziara ya naibu msaidi katika ofisi za waziri wa mambo ya nje wa Marekani John Sullivan mjini Khartoum.

Waziri wa mambo ya nje wa Sudan Ibrahim Ghandour alifahamisha kuwa katika mkutano waliofanya na mjumbe huyo kutoka Marekani, ushirikiano bain aya Korea Kaskazini na Sudan ulijadiliwa kwa kina.Habari Zinazohusiana