Korea Kusini yaongezeka kiwango cha tahadhari dhidi ya vitisho vya Korea Kaskazini

Korea Kusini imesema jumatatu kuwa imeongeza kiwango chake cha tahadhari kutoka na vitisho na uchokozi wa jirani wake Korea Kaskazini.

Kulingana na taarifa ya jeshi la Korea Kusini, wanajeshi wa Korea Kaskazini wamefyatilia risasi mmoja wa wanajeshi wao aliekimbilia Korea Kusini.

Taarifa hiyo ilisema kuwa ufyatulianaji wa risasi ulizuka pale wanajeshi wa Korea Kaskazini walipomuona mwanajeshi huo aliotoroka kwenye mpaka baina ya nchi hizo mbili, n kuongeza kuwa mwanajeshi huo alijeruhiwa na kupelekwa hospitali kupata matibabu.

Jeshi la Korea Kusini limesema kuwa liko tayari kukambiliani na vitisho vya Korea Kaskazini.

Ikumbukwe kuwa wanajeshi wawili wa Korea Kaskazini walitoroka nchi hiyo mwezi juni uliopita.

 Habari Zinazohusiana