Waziri mkuu wa Uturuki azungumza na waislamu wa Marekani

Waziri mkuu wa Uturuki asema kuwa hakuna tofauti iliopo baina ya wafuasi wa FETÖ na wanamgambo wa Daesh

Waziri mkuu wa Uturuki azungumza na waislamu wa Marekani

 

Waziri mkuu wa Uturuki katika ziara yake nchini Marekani alipokutana na waislamu alisema kuwa hakuna tofauti ilipo baina ya wafuasi wa kundi la FETÖ na wanamgambo wa kundi la Daesh.

Serikali ya Uturuki inatuhumu wafuasi wa kundi hilo kuhusika na jaribio la mapinduzi la Julai 15 mwaka 2016 nchini Uturuki.

Waziri Binali Yıldırım alitembelea  mskiti na jumba la utamaduni wa kiislamu nchini Marekani uliejengwa chini ya udhamini wa kitengo cha masuala ya dini cha Uturuki.

Kituo hicho cha utamaduni wa kiislamu kilizinduliwa Aprili 2 mwaka 2016  Maryland na rais wa Uturuki Recep Tayyıp Erdoğan.

Katika hotuba yake waziri mkuu wa Uturuki aliwaotolea wito waislamu kutoshirikiana na kwa hali yeyote na miliki za FETÖ ikiwemo shule na vituo vya utamaduni vya FETÖ.

Yıldırım alisema kuwa watu 250 walifariki na wengine zaidi ya 2 193 walijeruhiwa katika jaribio la mapinduzi la FETÖ.

 

 Habari Zinazohusiana