Uchambuzi wa matukio

Uchambuzi wa matukio

Uchambuzi wa matukio

Wale wanaoamini dini za Semavi, soma kitabu chako kitakatifu kwa fursa kubwa. Kama Mwislamu nina nafasi na fursa ya kusoma kitabu kitakatifu cha dini yangu. Ni maandiko matakatifu ambayo wanahistoria wote wa dunia wamesema kuwa aya zake na sura zake havijabadilishwa hadi sasa, na hili hunifanya kujisikia furaha sana.

Nina nafasi na fursa ya kusoma Qur'ani kila siku, ambayo ni kitabu changu kitakatifu .

Katika siku za nyuma nilipoisoma Qur'an, tukio la kihistoria nililokuta katika Surat ya Bakara lilinipa nguvu za kuendelea kuamini kitabu changu. Kwa sababu nililisoma katika kitabu kitakatifu cha Waislam, Wakristo na Wayahudi. Hadithi hiyo ilikuwa karibu sawa katika  vitabu vyote vitatu. Mbali na kusoma mamia ya maandiko ya kihistoria yaliyoelezea tukio hili, nilipata fursa ya kuona picha nyingi za kuchora, na sanamu zinazoelezea tukio hilo

Daudi na Jalut au Goliat wameelezewa katika aya tano kutoka aya 247 hadi 251 za Surah Al-Baqara katika Qur'an. Ni hadithi ya mtume Daudi, mtu mwenye nguvu sana na mnyenyekevu, na Goliat.

Katika Taurati, Samweli I na Samweli II, hadithi ya nabii Daudi na Goliat ni kama ifuatavyo:

"Daudi alionekana na kombeo na mawe machache dhidi ya Goliat. Kabla ya Goliat kushambulia, Daudi ghafla akajificha asiyeonekane, akirusha jiwe na kombeo lake na kuumiza Goliat chini ya paji la uso wake. Goliat alikufa pale pale, na Daudi kuwapa Waisraeli ushindi. "

Nikijaribu kuelewa na kwa mtazamo wangu, Goliat ana mita 3 za urefu. Ikiwa nabii  Daudi angemfuata na kumsogelea kwa karibu, kukabiliana nae ingekuwa kibarua kizito sana.

Michelangelo Merisi na Caravaggio ni wachoraji wa Milan.

Sijui kama umewahi kuona ubao unaoitwa "Daudi na Golyat" uliochorwa na Caravaggio mwaka wa 1610. Kama bado, basi ni Galleria Borgese huko Roma. Picha hii ni ya maajabu sana usipoangalia kiwiliwili chote. 

Caravaggio kuchora picha hii, ilikuwa ni kama kitendo cha kujitia kitanzi. Ilimbidi ahame Roma akimbilie mji wa Naples na miji iliyo karibu yake.  Mtu mwenye nguvu wa Kirumi, Kardinali Borgese, alijaribu kumsamehe.

Akifahamu jambo hili, Caravaggio alichora picha kama zawadi kwa Kardinali Borgese ili kumkumbusha kurudi Roma.

Caravaggio alifanya kazi hii kwa ufanisi. Ubao alipochora unamuonyesha Daudi mdogo, na jasiri, na unamuonyesha pia Goliat  mkubwa na wa kutisha kama hali yake ya sasa.

Mchoraji mkuu Caravaggio, kwa muda, anaelezea jinsi Daudi alivyogeuka kuwa Golyat. Kwa njia hii anaruhusu maovu ambayo yanachukua karibu kila nafsi yake ili kuvunja mawazo yake mabaya.

Kweli, hii ni picha ya dhamiri ya Carvaggio. Anatuambia kwamba aliua maovu yaliyo ndani yake na alitaka kusamehewa.

Picha hii katika Galleria Borgese inatualeza kuhusu  dhamiri yake, majuto, toba na uovu kwa maelezo yake.

Ni kipengele kikubwa zaidi na kizuri sana cha binadamu kujuta akiwa na huzuni wa moyo wake wote.

Katika ubao huo, ni Caravaggio wa leo, mwenye huruma  akimshtaki Caravaggio wa zamani mwenye dhambi.

Hebu angalia picha za wapiga picha au wachoraji, utawaona wakijipa uzuri. Lakini Carvaggio hakufanya hivyo, alijichora mwenyewe kwa kujipa mkono wa nabii Daudi. Ushahidi wa maumivu ya dhamiri katika picha pia umeandikwa kwenye  Upanga: "Unyenyekevu wa chini ni furaha."

Unasema nini kuhusu nabii Daudi, Carvaggio na viongozi wa sasa wa kisiasa? Kuna uhusiano wa karibu. Ikiwa Carvaggio angekuwapo leo, angechora hivi hivi raisi wa Marekani Trump, kansela wa Ujerumani Merkel, raisi wa Urusi Putin au kiongozi wa Irani Khamenei.

Viongozi hawa wote kwa bahati mbaya huchukua na kutekeleza maamuzi ambayo hufanya  kuendeleza nguvu zao za ulimwengu bila kujali.

Donald Trump, kwa mfano. Tangu siku zake za kutawadhwa kama raisi wa Marekani, ulimwengu umekuwa wa kushangaza. Anasukuma sera za ukatili za Marekani, kama alivyofanya Obama. Trump anataka Korea ya Kaskazini, Urusi, China, Iran, na hata Philippines wakiwa pamoja wapige magoti mbele ya Marekani.

Kansela  wa Ujerumani Merkel, ambaye amekuwa akitengwa, ni tofauti na Trump? Pia yeye anataka nchi  wanachama wa Umoja wa Ulaya ziwe kama majimbo ya Ujerumani. Uturuki, ambayo ni mshirika mkubwa zaidi  kibiashara na kisiasa wa Ujerumani, Angela anaitaka ikabidhi sera zake za usalama na siasa mikononi mwa Ujerumani.

Tukienda kidogo kwa Khamenei nae, yeye anataka ulimwengu wote wa Kiislam ujisalimishe kwa Iran.

Kuna majina ya manabii, wanafalsafa, wanasayansi na wavumbuzi ambao wanachangia maendeleo ya dunia. Nia za matarajio na hata siasa za maisha ya kibinadamu haziwezi kufikiria kuwa hawana sababu ya kufikiri juu ya kazi zao.

Ulikuwa na wasiwasi, Caravaggio alisamehewa?

Meli ilimuacha wakati wa mapumziko alipokuwa njiani kuelekea  Roma kwa ajili ya msamaha. Uchoraji wake ulikuwa mtaani. Alianza kukimbia ili awahi meli kwenye kituo kifutacho. Kwa bahati mbaya akafia njiani kabla hajafika. Lakini bado yu hai kwenye ubao akiwa na Daudi pamoja na Golyat...

 

 


Tagi: Goliath , Daudi

Habari Zinazohusiana