Uturuki na mtazamo wa Mashariki ya Kati

Uturuki na mtazamo wa Mashariki ya Kati

Uturuki na mtazamo wa Mashariki ya Kati

 

Mkesheka wa mwaka 2016 kuamkia 2017, kundi la DAESH lilifanya shambulizi za kinyama kwenye klabu mashuhuri ya mjini Istanbul, ijulikanao kwa jina Reina. Shambulizi hilo lilisababisha watu 39 kupoteza masiha yao.  Leo,  DAESH, mbali ya kuwa mashariki ya kati, kundi hilo la kigaidi leo linaendesha harakati zake hata Asia ya kati.

Mbali na mashambulizi ya DAESH katika maeneo mbalimbali ya dunia, leo swali linalojiulizwa, je DAESH  inajiandaa kuhamia katika nchi za Asia ya kati?

Pamoja na kwamba DEAŞ ina wapiganaji kutoka tabaka na makabila mbalimbali,  watu hujiuliza kuhusu wanachama wa DAESH wenye asili ya Uturuki. Katika majadiliano, mara nyingi hudai kuwa Asia ya Kati ni msingi / kituo cha DAESH mpya. Je, ni sawa? Tunataka kufafanua suala hili wiki hii.

DAESH imekuwa ikihusika na  mamia ya vitendo vya ugaidi hadi sasa. Hata hivyo, uraia na ukabila wamagaidi wanaoendesha mashambulizi ya kigaidi imekuwa maada kwenye ajenda. Kwa nini? Kabla ya kujibu swali hili, hebu tuangalie kwenye utafiti uliofanya kuhusu uraia wa wanachama wa kundi la DAESH .

Kulingana na takwimu zilizochapishwa mnamo Machi 2016, nchi kumi zenye raia wake kama wanachama wa DAESH ni kama ifuatavyo:

 

 

Tunisia

6500

Suudi Arabia

2500

Urusa

2400

Jordan

2250

Uturuki

2100

Ufaransa

1700

Morocco

1350

Libnan

900

Misri

800

Ujerumani

760

 

 

 

 

Kulingana na utafiti uliochapishwa mwaka 2015, kwa kila raia milioni moja, hiyi ni orodha ya wapiganaji wa DEASH katika nchi zifuatazo:

 

 

Jordan

315

Tunisia

280

Suudi Arabia

107

Bosnia

92

Cosovo

83

Türkmenistan

72

Albania

46

Ubelgiji

46

Uzbekistan

33

Uswidi

32

Palestina

28

Danmark

27

Tajikistan

24

Ufaransa

18

Austria

17

Uhoolanzi

15

Finland

13

Urusi

12

Kazakistan

8

Utruruki

6

Kırgızistan

5

 

 

 

Kuna utafiti kadhaa uliofanywa kuhusiana na wapiganaji wa DAESH. Sisi tu tulichukua mbili kama mifano. Hakuna data sahihi inayohusiana na mada hii . Hata hivyo, inawezekana kwamba tunaweza kuwa na maoni ya jumla kutoka kwa utafiti uliofanywa. Takwimu zingine zimechapishwa pia kwenye mtandao.

Tunapoangalia  takwimu, tunaona kwamba ni karibu nchi zote za dunia, na inadhihirika kuwa uwepo wa DEASH katika nchi za Asia ya kati sio wakupuuzia. Hata hivyo, kiwango hiki cha ushiriki kwa DAESH ni cha chini sana ikilinganishwa na nchi za Balkan kama Bosnia, Kosovo, Albania , nchi za Ulaya, Mashariki ya Kati, na nchi za Afrika Kaskazini kama Tunisia.

Hata hivyo, katika viako vya kikanda na vile vya kimataifa, magaidi kutoka Asia ya Kati huzungumziwa daima. Baadhi ya sababu kuu za hivi ni: baadhi ya nchi za Asia ya kati huwapa uhalali fulani wanaohusika na harakati za kigaidi sababu serekali hizi huzungumzia kila siku hofu ya makundi haya na hii huweza kuvutia umakini wa raia. Propaganda hii za baadhi ya serekali, hutumiwa ili wawezekudhibiti au kunyanyasa raia zao. Utawala huu ni mwanzo wa wale ambao hueneza propaganda hii. Baada ya mashambulizi ya Septemba 11 huko Amerika, Jamhuri ya Watu wa China ilitangaza au ilihisha jamii ya Uiguri na itikadi kali. Hata hivyo, kabla ya Septemba 11, hatukuwahi kusikia jamii ya Uighur ikihusishwa na vitendo vya kigaidi au vya itikadi kali.

Hivyo propaganda hii inakuja nchini China, na China ni kati ya wale ambao hueneza propaganda hii.  Urusi nayo imeanza kuchukuwa na kuongelea propaganda hii , kwa sababu lugha hii inaimarisha uwepo wa Urusi katika Asia ya kati kama jukumu lake la kulinda amani na usalama wake. Inahalalisha sera za Urusi kuelekea Asia ya Kati. Baadhi ya wataalam wa kigeni ambao hawajui hali halisi ya Asia ya Kati huchangia  moja kwa moja kueneza na kukubalika kwa propaganda hizi. Kuna hata makundi mengine yanayoeneza propaganda hizi kwa madhumuni mbalimbali ya kisiasa na kiitikadi. Tunaona hii hasa Uturuki. Makundi mbalimbali ambayo yamechanganyikiwa na sera mbalimbali za Uturuki za kujitegemea na utamaduni wa Uturuki kuelekea Asia ya Kati hueneza propaganda hii hasa.

Matokeo yake, "Kuna tishio la DAESH katika Asia ya Kati?" "Ndiyo, lipo." Hata hivyo, "Je, tishio la DEASH kwenye kanda ya  Asia ya Kati  ni chumvi kwa maoni ya umma wa Uturuki na ulimwengu? "Jibu letu itakuwa" hapana, hakuna ".


Tagi: DAESH

Habari Zinazohusiana