Uchambuzi wa matukio

Uchambuzi wa matukio

Uchambuzi wa matukio

 

Mkutano muhimu ulifanyika nchini Uturuki wiki iliyopita. Jina la mkutano huo ni Baraza la Kimataifa la Ustaarabu.

Hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Uturuki Erdogan iliyotolewa katika mkutano huo, ilikuwa ni kumbukumbu muhimu sana. Sijawihi kuona mtu wa ulimwengu wa Magharibi aliyewahi kutowa hotuba kama hiyo kwa sababu ulimwengu huo unastahiki maadili yake. Lakini, bila shaka wataanza kusema juu yake, watajidili kikamilfu, na kuandika maandiko.

Rais wa Uturuki, Erdogan, aliniacha mdomo wazi, mimi kama mwandishi, kuelezea hadithi ya ustaarabu huu, ambayo ilipaswa kuchunguzwa na wachunguzi, waandishi na wasomi.

Mheshimiwa rais Erdogan, kwa muhtasari katika mkutano alisema, na hapa namnukuu:

Sisi tuko kwenye mapambano ya ustaarabu. Sisi tuko kwenye harakati za kujenga ustaarabu. Kwa kuwa  imani ndiyo inao amua asili ya ustaarabu, basi tunapaswa kubadili tofauti zetu. Jina la kile kinachojitokeza wakati unapopuuza imani na ushirikiano wa kijamii , sayansi na teknolojia kuwa muhimu siyo ustaarabu kwetu. Katika ustaarabu wetu, mtu ni kiumbe cha heshima zaidi. "

Maendeleo katika haki za binadamu zote, ambazo hazijazuiliwa na ulimwengu wa magharibi tangu miaka ya 1950, zinatia hofu na huzuni.

Rais Erdoğan pia alipaza sauti katika mkutano huo. Leo, kama maslahi ya Magharibi yako hatarini, basi demokrasia, azimio la Umoja wa Haki za Binadamu, na sheria havina maana.

Kwa mfano, ulimwengu wa Magharibi, umesimama kidete  nyuma ya kura ya maoni kinyume na sheria  iliopigwa kaskazini mwa Iraq, wakati huo huo wamepinga kura ya maoni jimboni Catalonia  Uhispania.

Ulimwengu wa magharibi umebaki kimya dhidi ya uamuzi haramu wa Jaji wa Uhispania kuhusu siasa za Catalonia. Na hiyi ni sahihi kwao kufimbia macho siasa za Catalonia sababu ni mingoni mwa maslahi yao.

Serikali ya Uhispania, ambayo haikufurahishwa na kura hiyo, ilichukua uamuzi wa kuitisha uchaguzi mwingine ndani ya kipindi cha miezi sita, na kufutilia mbali serikali ya uhuru ya Catalonia. Kama nilivyosema, tukio hilo lipo katikati ya maji yao, na linafaa kwa maslahi ya magharibi.

Nini kilichotokea Magharibi? Nini kilichotokea kwa mtaalamu wa Magharibi ambaye alishinda Roma, Kaisari, madikteta wakuu, na wafalme ?

Ikiwa ni Magharibi au Mashariki, kama wanavyuoni wenye akili wanasubutu kukaa kimya , au wanaamua kutozungumza , basi uwiano wa dunia hupotea. Wajuwe kuwa majeshi ya Magharibi yameua watu milioni 4  Mashariki ya Kati tangu 2001. Asilimia 80 kati yao walikuwa wanawake, watoto, na raia wa kawaida. Je, wasomi wa magharibi walipinga?

Hitler, Mussoloni, Stalin, Churchill, kama vile kilichotokea kwa wafuasi wa wasomi waliopambana na ukatili wao. Leo katika ulimwengu wa magharibi, ni watu wangapi wanaandika kitu kwa jina la falsafa. Hata makala za gazeti zinasomwa na watu wawili au mia tatu. Hii ni hali mbaya kwa kweli kuwahi kutokea.

Hali ya ulimwengu wa Mashariki nayo sio nzuri sana. Mawazo yanayomulikia wanavyuoni hayakuwa mabaya kama ilivyo katika Magharibi, lakini hayasomwi kwenye kiwango kinachohitajika.

Ushirikiano wa ajabu na kuingilia kati kwa Uturuki kumedhoofisha kundi la kigaidi la DAESH. Kundi hilo la kikatili na wafadhili wake hawana nafasi ya kuishi katika kanda yetu. Kuna maelfu katika wafuasi na wasimamizi wa DAESH ambao walitoka ulimwengu wa Magharibi , na wanachama hao DAESH ikishafyekwa watarudi kwao.

Watakuwa chanzo cha shida kwa kiwango kikubwa katika nchi zao wenyewe. Ukatili na kuongezeka kwa unazi, vinavyochochewa na mbinu za siasa za Magharibi, vitapambana na ufahamu mwingine wa kigaidi wa watoto wao wenyewe.

Mgogoro huu utaitingisha jamii yote ya Magharibi. Katika ulimwengu wa magharibi, tunasubiri na tutaona pamoja demokrasia dhidi ya watoto wa kigaidi, na pia uharibifu wa tamaduni za  Mashariki pamoja na demokrasia kwa maslahi yao wenyeweHabari Zinazohusiana