Uturuki na mtazamo wa Mashariki ya Kati

Uturuki na mtazamo wa Mashariki ya Kati

Uturuki na mtazamo wa Mashariki ya Kati

 

Kufuatia kura ya maoni ya kujitenga iliopigwa kwenye  jimbo la wakurdi la Iraq , serikali ya Iraq ilipinga kura hiyo kwa mujibu wa sheria ya kimataifa na imeanza kurejea mipaka yake ya  2003.

Je, hatua hii ilienda aje? Hebu tukumbuke kwa ufupi: DAESH ilipoibuka utawala wa Baghdad ulidhohofika. Jimbo la wakurdi la Iraq lilitumia fursa hiyo na kuvuka imipaka na mamlaka linalopewa na katiba. Vikundi vya jimbo hilo  vilijipa udhibiti kamili wa Kirkuk, na viliimarisha uwepo na nguvu zao katika mikoa mingine yenye utata. Barzani alifaidika kutokana na udhaifu wa serikali kuu ya Iraq . Serekali ya jimbo hilo ilishikilia sehemu nyingi kutoka mikononi mwa DAESH kuanzia Sincar hadi Hanekin  kwa usaidizi wa operesheni za anga za umoja wa kimataifa. Serekali ya jimbo hilo ilitangaza kuwa itaongeza maeneo hayo kwa jimbo hilo inalodhibiti na haitaondoka. Kura ya maoni imekuwa kikomo kwa hatua hiyo.

Licha ya upinzani dhidi ya kura ya maoni, Barzani alisonga mbele na uamuzi wake ulionekana kama ushindi mkubwa juu ya misingi yake mwenyewe. Hasa, Barzani na baadhi ya nchi za Magharibi ambazo zinamuunga mkono walidhani kuwa  kura hii itawapa uhuru kamili, na baadae hatua za kukabiliana na uamuzi wao zilianza kujitokeza. Serikali ya Iraq iliendelea kufanya taratibu za kisheria nchini, huku ikiionya serekali ya jimbo la wakurdi  kufuta kura ya maoni. Katika kipindi hiki, mazungumzo ya ngazi ya juu yalifanyika kati ya Uturuki na Iran. Kutokana na mazungumzo haya, kulikuwa na msaada kamili kwa serikali ya Iraq. Katika mfumo huu, serikali ya Iraq imeanza kuchukua hatua dhidi ya kura hio. Hatari ya kuzuka vita baina ya serekali ya Iraq na jimbo hilo ambalo baadae lilianza kurudi kwenye mipaka yake ya 2003.

Siku moja kabla ya kuingilia kati, peshmerga walianza kukimbia wakitoroka huku wakivua sare rasmi barabarani wakati mapigano halisi yalipoanza. Bendera ya serikali kuu ya Iraq ilitiwa tena kwenye majengo rasmi. Ishara zote za serekali ya jimbo la wakurdi la Iraq zilipigwa chini. İmekuwa ni ishara ya kuanguka kwa utawala wa jimbo hilo kwenye mikoa ya Kirkuk.

Kirkuk iliingia mkataba na serikali ya Iraq, udhibiti wa jeshi la Iraq na Hashti Shabi. Mikoa mingine ya utata ilianza kufanya mabadiliko ya haraka. Vikosi vya Iraq vilichukua udhibiti kutoka Kirkuk kwenda mashariki, maeneo ya utata huko Tuzhurmatu na Diyala. Katika magharibi, jeshi la serikali ya Iraq  limesonga mbele kwa kasi katika maeneo ya kaskazini na magharibi mwa mkoa wa Mosul.

Barzani ni mshukiwa mkubwa wa hali inaokumba jimbo la wakurdi la Iraq. Uturuki na Iran hawakutambua kamwe  kura ya maoni ya kujitenga kwa wakurdi. Barzani hakuweza kutafakari  nguvu za kijeshi na za kisiasa zake. Alichukulia usaidizi wa magharibi  zaidi kuliko nguvu zake, na alikuwa na uaminifu sana na nchi hizo za magharibi.

Kwa upande mwingine, Uturuki ilitangaza kuwa itawasiliana moja kwa moja na serikali kuu ya Iraq kuhusu mpaka wa Iraq. Inaeleweka kuwa mpaka mpya utajengwa na mpaka wa zamani utawasilishwa kwa Baghdad. Lakini swali pekee kwa Uturuki sio Kirkuk au mikoa ya utata. Uturuki ina wasiwasi kwamba pengo lililoachwa na serekali ya jimbo la wakurdi wa Iraq huenda ikachukuliwa na kundi la kigaidi la PKK.

Hata hivyo, mchakato huu pia unaweza kuimarisha PKK nchini Syria, pamoja na ushawishi wake nchini Iraq.Habari Zinazohusiana