Pentagon yathibitisha kuuawa wanajeshi wake nchini Niger

Msemaji wa Pentagon, Meja Michelle Baldanzi , amethibitisha kuwa shambulizi lililowauwa askari wa Marekani nchini Niger, liliendeshwa na kundi la Daesh

Pentagon yathibitisha kuuawa  wanajeshi wake nchini Niger

Msemaji wa Pentagon, Meja Michelle Baldanzi , amethibitisha kuwa shambulizi lililowauwa askari wa Marekani nchini Niger, liliendeshwa na kundi la Daesh . Meja Michelle alijiziwia kutoa taarifa kamili kuhusiana na shambulizi hilo kutokana na upelelezi unaoendelea.

Afisa wa wizara ya ulinzi alipokwa akihojiana na vyombo vya habari, alisema kuwa magaidi 15 ndiyo waliotekeleza shambulizi la Oktoba 6 nchini Niger.

Kamanda wa vikosi vya Marekani, anayehusika na operesheni kwenye nchi za Afrika, alisema kuwa askari wa Marekani walishambuliwa walipokuwa njiani kutoka kwenye mkutano na viongozi wa makabila kwenye mpaka wa Niger na Mali .

 Habari Zinazohusiana