Uturuki na mtazamo wa Mashariki ya kati

Uturuki na mtazamo wa Mashariki ya kati

Uturuki na mtazamo wa Mashariki ya kati

 

Iran na Uturuki ni nchi ambazo zinapakana na  zenye mpaka wa kilomita 560 kati yao. Uturuki tayari ina ubalozi ya kwenye miji tofauti ya Tehran, ikiwemo Tabriz, Urumiye na Makarudha. Iran ina balozi wake  nchini Uturuki mjini Ankara pamoja na Istanbul, Erzurum na Trabzon.

Uturuki inalenga kuendeleza mahusiano na Iran, siyo mahusiano ya kuingiliana kwenye mambo ya ndani, bali kuendeleza heshima na kanuni nzuri za kikanda.

Hasa jitihada zinafanywa ili kuimarisha uhusiano huo na kuutatua mizozo ya kikanda, na ziara za ngazi ya juu zimefanyika katika kipindi hiki.

Moja ya tukio lililoleta hizi nchi mbili kuimarisha urafiki sana ni kura ya maoni ya hivi karibuni kwenye jimbo la wakurdi la Irak.

Watafiti wa mambo ya kisiasa wanatathmini kuwa ukaribu huyu wa Iran na Uturuki ni muungano mpya katika mashariki ya kati. Ni mapema mno kuelezea uhusiano huu kama muungano.

Hata hivyo, haishangazi kuwa uhusiano kati ya nchi hizo mbili huenda utakuwa muungano imara.

Kwa miaka mingi, Uturuki na Iran wamekuwa wakishindana  katika eneo kubwa kutoka Caucasus hadi Asia ya Kati na kisha Mashariki ya Kati, hadi katika eneo la  Asia ya Kusini Mashariki. Mashindano yenyewe bado hayajafika mwisho.

Hata hivyo, sisi pia tunajua kwamba serikali hizi mbili zinashirikiana kwenye nyanja za uchumi na biashara kama vile RCD, D-8, ECO na nyanja  za usalama kama vile Sadabad Paktı na Baghdad Paktı.

Ziara ya hivi karibuni ya Rais wa Uturuki, Recep Tayyip Erdogan, nchini Iran imesisitiza uhusiano wa Uturuki na Irani katika kanda hii ya Mashariki ya Kati .

Ziara ya amiri jeshi mkuu wa Uturuki, Hulusi Akar, nchini Iran, na ziara ya waziri mkuu wa Irani, Muhammad Bakiri,nchini Uturuki mwezi mmoja kabla ya ziara ya Erdogan zimeimarisha uhusiano wa nchi hizi.

Leo, bila shaka,migogoro ya Irak na Syria inaleta pamoja Ankara na Tehran. Msimamo wa pamoja wa Uturuki na Iran dhidi ya kura ya maoni ya jimbo la wakurdi la Irak umeweza kuanzisha ari na zama mpya baina ya nchi hizi mbili katika sekta nyingi tofauti .

Ankara na Tehran wameamua kurudi pamoja kutokana na makosa ya Barzani na wameafikiana kuisaidia Baghdad dhidi ya Erbil.

Mazungumzo ya Erdoğan na viongozi wa Iran  Tehran yamethibitisha haya.

Kwa mfano, ni muhimu kuona kwamba Erdoğan ana msimamo wa pamoja na viongozi wa Iran kwamba Israel na Marekani wana ushawishi wao juu ya maamuzi ya Barzani.

Iran na Uturuki waliamua kuwa vikwazo dhidi ya Erbil viongezwe na viendelee.

Uturuki na Iran sasa wanafahamu vitisho vinavyowakabili katika kanda yao. Kwa sababu hii, ukaribu baina yao utaendelea.

Masuala ya usalama wa nchi hizi mbili yanaongeza kasi ya ushirikiano wao. Ugomvi wa kupigania ubabe wa kikanda kati ya nchi hizi mbili, hasa  Syria na Irak ulifanya kundi la PKK kujidhatiti na kuimarisha ngome zake.

Je! inawezekana Ankara na Tehran kuacha na kutupilia mbali uhasama wao ili kuangazia ushirikiano wao unaoanzishwa ? Hii itaborosha siasa na hali nzima ya kanda.

 Habari Zinazohusiana