"Ushirikiano wetu na Uturuki haujaathirika"

James Mattis asema kuwa ushirikiano baina  ya Uturuki na Marekani haujaathirika

"Ushirikiano wetu na Uturuki haujaathirika"

 

James Mattis asema kuwa ushirikiano uliopo baina ya Marekani na Uturuki haujaathirika na mzozo wa viza kati ya mataifa hayo.

Waziri wa ulinzi wa Marekani James Mattis asema kuwa mzozo wa kusitishwa zoezi la utoaji viza kwa raia wa Uturuki na raia wa Marekani haujathiri ushirikiano uliopo baina ya Uturuki na Marekani.

Hayo waziri wa ulinzi wa Marekani James Mattis aliyazungumzo akiwa safarini akielekea Florida na waandishi wa habari.

Mattis amesema kuwa  Uturuki ni mshirika na mwanachama wa NATO na kuendelea ushirikiano na mazungumzo.

Jeshi la NATO linaushirikiano na jeshi la Uturuki katika mawasiliano na matukio ya Syria, Iraq na Kusini mwa Uturuki.

Kambi ya Incırlık ya jeshi la NATO ipo wazi kwa ajili ya kupambana na adui.

 Habari Zinazohusiana