Rais Erdoğan amesema kuwa wakoloni ndio wanaoisambaratisha Iraq na Syria

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdoğan amesema kuwa wakoloni wanatumia njia ya kusambaratisha na kutawala majimbo tofauti nchini Syria na Iraq.

Katika mkutano mjini Ankara,rais Erdoğan amesema kuwa kama ilivyokuwa ikifanywa zamani na makundi ya wakoloni waliokuwa wakisambaratisha nchi tofauti kwa nia na dhumuni la kuzitawala ndivyo ilivyo sasa hasa kwa Syria na Iraq.

Kwa mujibu wa habari,rais Erdoğan amesema kuwa kuna makundi yana nia ya kuzisambaratisha Syria na Iraq na mwisho kuzingira kusini mwa Uturuki.

Rais Erdoğan amezidi kukemea kura ya maoni ya Iraq na kusema kuwa huo ni mwanzo tu.

25 Septemba,jimbo la Wakurdi kaskazini mwa Iraq  lilipiga kura ya maoni ya kujitenga na Iraq.Habari Zinazohusiana