Obama asisitiza njia ya mazungumzo kati ya Marekani na Korea Kaskazini

Rais wa zamani wa Marekani Barack Obama amesema kuwa njia muhimu na sahihi ya kutatua mzozo kati ya Korea Kaskazini na Marekani ni diplomasia.

Kiongozi huyo wa zamani ameyazungumza hayo wakati wa mkutano nchini Brazil.

Obama amesisitiza na kusema kuwa,vitisho na ndege za kivita havitasaidia kutatua mgogoro huo.

Aidha Obama amesema kuwa enzi za utawala wake,nchi iliyokuwa ni tishio kubwa kwa Marekani katika masuala ya mabomu ya Nyuklia ni Iran.

Hata hivyo Marekani na Iran zilihakikisha zinafikia makubaliano ili kutoruhusu utengenezaji wa makombora ya nyuklia.

Rais wa sasa Donald Trump anaonekana kutotumia diplomasia hata kidogo wakati akizungumza na kiongozi wa Korea Kaskazni Kim Jong Un.

Bwana Obama pia ameongeza kwa kusema kuwa anasikitika kuona kuwa amemaliza muda wake kama rais wa Marekani bila ya kuweza kumaliza tofauti za kisiasa kati ya watu tofauti nchini humo.Habari Zinazohusiana