16 wafariki baada ya basi kugongana na treni Urusi

Watu 16 wameripotiwa kufariki baada ya treni kulivaa basi lililokuwa limeharibika katika moja ya barabara karibu na Moscow.

16 wafariki baada ya basi  kugongana na treni Urusi

Watu 16 wameripotiwa kufariki baada ya treni kulivaa basi lililokuwa limeharibika katika moja ya barabara karibu na Moscow.

Kwa mujibu wa habari,basi hilo lililokuwa limebeba wafanyakazi kutoka Uzbekistan lilikuwa limeharibika wakati treni ikilivaa na kusababisha vifo vya watu 16.

Baadhi ya abiria walikuwa wakijaribu kulisukuma basi wakati ajali ikitokea.

Ripoti zinaonyesha kuwa basi hilo lilikuwa na leseni ya Kazakhstan.

Uchunguzi zaidi unaendelea.

Tagi: basi , treni , ajali , Urusi

Habari Zinazohusiana