Uturuki na mtazamo wa mashiriki ya kati

Uturuki na mtazamo wa mashiriki ya kati

Uturuki na mtazamo wa mashiriki ya kati

 

Mipakani kusini mwa Uturuki, tarehe 24 August ilianzishwa operesheni ya kijeshi ya Fırat Kalkanı Operasyonu (FKO) ambayo madhumuni yake ilikuwa ni kufyeka makundi ya kigaidi ya DEAŞ na PKK.

Operesheni hiyo iliwapa pigo kubwa DEAŞ na PKK, na pia imeweza kuwazuwia PKK kuingia kanda za Mediterranea.

Baraza la usalama la Uturuki lilitangaza manamo tarehe 29 Machi 2017 kumalizika kwa operesheni hiyo iliyodumu takriban miezi saba na kuongeza kuwa operesheni za kijeshi kama hizi zinaweza zikaanzishwa mda wowote ule hata kwenye kandi nyingine.

FKO iliyoendeshwa na Jeshi la Uturuki (TSK) ikishirikiana na  Jeshi la Uhuru wa Syria (ÖSO). Mnamo tarehe 24 Agosti, 2016, magari ya kivita ya jeshi la Uturuki yaliingia katika eneo la waturkmen la Cerablus. Operesheni ya FKO ilikuwa na malengo mawili .

La kwanza ilikuwa kufukuza DEAŞ mbali na mpaka wa Uturuki na kufyeka kundi hili la kigaidi. La pili ilikuwa ni kuzuwia PKK kuimarisha ngome zake kaskazini mwa Syria.

Malengo yote mawili ya operesheni hii ya FKO yamefanikiwa. Kwa hiyo, operesheni ya FKO ilizuia kunda la kigaidi DEAS kuendesha mikakati yake, pamoja na kuzuia kundi la PKK kuanganisha maeneo iliokua ikikalia.

Operesheni ya FKO iliweza kurudisha maeneo yaliokuwa yameshikikiliwa na makundi ya kigaidi yenye kilomita 2300 za mraba hasa maeneo ya Azep, Bab, Azep, Bab, na Cerablus yanayopatikana kaskazini mwa Alepo.

Miaka minne imeanea, raia wakiteswa na DEAŞ. Lengo lingine la FKO ni kujenga eneo salama katika kanda hiyo ili maisha yarudi kuwa kawaida kama zamani. Eneo hili litawapokea wale wanaokimbia unyanyasaji wa serikale na wale wanaotaka kurudi nchini.

Ingawa operesheni ya FKO imefanikiwa , hali ya kisiasa na ya kibinadamu bado ni tata. Miradi ya kiraia ilifanyika katika maeneo ya  Cerablus, Chobanbey, Bab na Azez. Na matunda ya miradi hiyo yameonekana baada ya utafiti ulioendeshwa.

Hata hivyo, kuna ongezeko la idadi ya watu katika eneo kutokana na waliotoka mikao mingine. Si jambo rahisi kuboresha maisha ya kila siku haraka sana katika mazingira ambao uwezekano wa uzalishaji ni mdogo na sehemu kama hiyi ambayo shughuli za kiuchumi zinahitaji msaada wa kuendelea.

Eneo hili  linahitaji wakati ili kujikwamua. Kwa msaada wa Uturuki, kanda hiyi imekuwa eneo salama na lenye  ulinzi mkubwa.

Hata hivyo, uchumi na maisha ya raia vinahitaji miaka ili kustawi katika eneo hili. Maisha yanaweza kurejea  upya kupitia hatua za kiraia kama ilivyofanyika katika operesheni FKO.

Katika hali hii, kuna mambo mengi ambayo Marekani na Urusi zitajifunza kutoka operesheni ya FKO.

Tarehe 24 Agosti 2016, Jamhuri ya Uturuki ililazimika  kuingia katika awamu ya vita moja kwa moja, sababu ilikuwa muhimu katika mapambano dhidi ya DEAŞ.

Kwa mujibu wa sheria ya kimataifa, Uturuki iliingia katika vita hiyo kwa kuzingatia kifungu 51 cha Mkataba wa Umoja wa Mataifa, kinachoiruhusu Uturuki kujihami dhidi ya DAEŞ ilioshambulia maeneo ya Uturuki.

Kutokana na msaada wa kijeshi wanaohitaji ÖSO na Turkmen, imethihirika kuwa wao wanaweza kuwa washirika wazuri dhidi ya DEAŞ. Majimbo yaliokombolewa kutoka mikononi mwa magaidi yanaweza yakalindwa na kuwa na usalama wa kutosha, na imedhihirika kuwa kundi la kigaidi haliwezi kushirikishwa au kutumiwa katika vita dhidi ya kundi lingine la kigaidi.

FKO inaweza kuchukuliwa kama hatua ya kwanza ya vita dhidi ya ugaidi inayoendeshwa na Uturuki na washirika wake.

Kwa Uturuki, tishio kubwa la mipaka yake na usalama wa ndani hutoka kwa kundi la  PKK nchini Syria baada ya kung,olewa kwa DEAŞ mipaka.

Awamu za FKO bila shaka zitalenga PKK / PYD / PLO. Ni katika muelekeo huu, uamuzi wa utawala wa Marekani wa kuwapa silaha PKK, na kushirikiana kwao kwenye operesheni ya Rakka, na kujaribu kuzuia mgongano kati ya Uturuki na PKK kaskazini, inaonekana kuwa ni mojawapo ya matatizo makubwa baina ya Uturuki  na Marekani.

 Habari Zinazohusiana