Rais Erdoğan kuelekea Ujerumani mwezi Julai

Rais Recep Tayyıp Erdoğan atarajiwa kuzuru nchi ya Ujerumani mwezi Julai

Rais Erdoğan kuelekea Ujerumani mwezi Julai

Rais wa Uturuki Recep Tayyıp Erdoğan atarajiwa kuzuru Ujerumani ifikapo mwezi Julai.

Vyanzo vya habari vya urais siku ya Jumatatu vyafahamisha kwamba rais Erdoğan atatekeleza ziara rasmi Ujerumani kati ya tarehe 7 na 8 mwezi Julai.

Kumekuwa na hali isiyokuwa na maelewano baina ya Uturuki na Ujerumani hasa kuhusu suala la wabunge wa Ujerumani kuzuru askari wao katika kambi ya İncirlik iliyoko nchini Uturuki.

Uturuki imewanyima wabunge hao hasa wa chama Die Linke nchini Ujerumani ambao wanaunga mkono kundi la kigaidi la PKK.

Maelezo zaidi kuhusu ziara ya Erdoğan Ujerumani yatatolewa .

 Habari Zinazohusiana