TRT Redio

TRT REDIO

Kawaida huwa tunalalamika kwa kuwa maendeleo ya kisayansi na teknolojia hutufikia kwa kuchelewa nchini mwetu. Hata hivyo,  madai haya ni kinyume kwa upande wa redio. Tajriba ya redio ya jamii ya Kituruki ilianza wakati mmoja sawa na dunia ya tarehe 6 mwezi Mei mwaka wa 1927. Kasi mpya ilizidi kuongezeka baada ya uanzilishi wa Idhaa ya Redio na Runinga ya Kituruki ya (TRT) tarehe 1 Mei mwaka 1964.

Hadi kufikia sasa, vituo vya redio ya TRT vimejizatiti kufikia tabaka mbali mbali za jamii katika kila pembe ya nchi kwa kuwajibika katika utangazaji wa umma na kuzingatia ufahamu wa lengo na kanuni za utangazaji, kwa ufasaha wa lugha ya Kituruki katika mikusanyiko ya taarifa za habari za kuelimisha, utamaduni, muziki na burudani.

Matangazo ya Redio ni nguvu ya ufanisi katika nchi yetu na dunia kupitia vituo vya redio za Kituruki za TRT; Radio-1, Radio-2 (TRT FM), Radio-3, Radio-4, vituo 5 vya redio za mikoani (Antalya, Çukurova, GAP-Diyarbakır, Erzurum, Trabzon), TRT Melody kwa wale wanaopenda miziki ya jadi ya Kituruki, TRT Folk song kwa wapenzi wa miziki ya asili, TRT Radio News Channel (Idhaa ya taarifa za habari) na vituo vya redio za kimataifa, The Voice of Turkey Radio (Redio ya Sauti ya Uturuki inayorusha matangazo kwa lugha 32) na Europe FM (Idhaa ya Ulaya).

Radio 1, ni idhaa inayoelimisha, ya utamaduni na taarifa za habari. Vile vile ni idhaa ya watu wote wanaohitaji taarifa na elimu. Matangazo hufanywa muda wote. Inarusha matangazo yake kote nchini kwa kutumia mamia ya visambazio na kusambaza dunia nzima kupitia satelaiti na mtandao. Sayansi, sanaa, fasihi, michezo ya kuigiza, michezo, mazingira, uchumi, taarifa maalum na mengine yote yanayohusiana na maisha. Taarifa sahihi, zenye malengo na matangazo ya haraka.

TRT Radio1

Kutoka mwaka 1927 hadi kufikia leo… Kila sehemu iliyokuwa na redio.

 

Radio-2 (TRT FM), inarusha matangazo muda wote kila siku kwa mfumo wake wa kipekee wa TRT ulio bora. Ni ya kusisimua na kufurahisha.

Nyimbo zilizoko kwenye chati na zinazovuma. Matangazo yake yanarushwa kote nchini Uturuki kwa kutumia mamia ya visambazio na kusambaza dunia nzima kupitia satelaiti na mtandao. Inafikia asilimia 99.9% ya eneo zima. Ni msiri wako, rafiki yako na msafiri mwenzako.

TRT FM

Ni idhaa ya redio inayopunguza masafa.

 

Radio-3, inatoa mifano ya miziki iliyovuma kwa upana kuanzia ya Elvis Presley mpaka Joan Baez, Frank Sinatra hadi Thaikowsky na Mozart pamoja na Sara Vaughan kwa kujumlisha miziki ya jadi na ya kisasa. Idhaa inarusha matangazo muda wote kwa mfumo wa kipekee wa TRT ulio bora. Inafikia kila pembe ya Uturuki kwa kutumia mamia ya visambazio na kusambaza dunia nzima kwa njia ya satelaiti na mtandao.

TRT Radio 3

Ni bora katika Muziki

 

Radio-4, maua ya muziki wa asili na kitamaduni yanapatikana katika bustani hii. Muziki wa asili ya Kituruki aina ya Saz Semai unaopigwa kwa kutumia vyombo vya asili ya kituruki vya Saz vilivyotengezwa kwa nyuzi , Longa ambao ni aina ya muziki wa Kituruki, vitangulizi vya miziki, nyimbo mbali mbali za mapenzi na kuliwaza, Horlat na kitamaduni za Anatolia. Waimbaji na wapigaji chombo cha Saz stadi wa zamani na wa sasa. Wote wanapatikana katika kituo hiki. Idhaa hii inarusha matangazo muda wote kwa mfumo wa kipekee wa TRT ulio bora. Inafikia kila pembe ya Uturuki kwa njia ya visambazio na kusambaza dunia nzima kupitia satelaiti na mtandao.

TRT Radio 4

Ni kituo ambapo hamu yako inapoishia.

 

 

TRT Folk Song ni kituo kilichoanza utangazaji tarehe 1 Julai mwaka 2009 kwa madhumuni ya kuwaburudisha wapenzi wa nyimbo za asili kupitia visambazio vya FM, statelaiti na mtandao. TRT Folk Song huzidisha hamu ya wasikilizaji wa miziki ya asili ya Kituruki kwa kucheza nyimbo za asili za kipekee zilizovuma muda wote. Miongoni mwa nyimbo hizi za asili ni zile zinazodumisha na kutangaza mila na utamaduni wetu.

 

TRT Nağme, tangu kuanza utangazaji tarehe 6 Mei mwaka 2009, TRT Nağme imewakidhi wapenzi wa muziki wa jadi wa Kituruki kupitia visambazio vya FM, statelaiti na mtandao. TRT Nağme inacheza miziki ya jadi ya Kituruki masaa 24. Nyimbo maalum zilizochaguliwa kutoka kwenye hifadhi ya TRT pamoja na nyimbo mpya zilizorekodiwa zinaweza kusikilizwa katika kituo cha TRT Nağme.

 

TRT Radio News, matangazo ya redio za mikoani Antalya, Çukurova, GAP-Diyarbakır, Erzurum na Trabzon hupeperushwa hewani kati ya saa 10.00 – 13.00 kila siku yanayotoa habari na taarifa zinazohusu maendeleo na masuala katika mikoa hiyo. Katika matangazo ya ‘’Anadolu Kuşağı’’ yanayofanyika baada ya saa 13.00 kwenye kituo cha TRT Türk, kila kituo cha redio za mikoani hutoa simulizi za hadithi na burudani ya miziki kote nchini.

 

Voice of Turkey (Sauti ya Uturuki)… Kutoka Radio Ankara (Redio ya Ankara) hadi (Sauti ya Uturuki) Voice of Turkey kupitia nyuzi za usambazaji. Voice of Turkey (Sauti ya Uturuki) imesikika kote dunia nzima kwa kipindi cha zaidi ya miaka 70. Habari, michezo, utamaduni na sanaa, muziki na burudani… Voice of Turkey (Sauti ya Uturuki) ni kiunganishi baina ya raia wa Kituruki wanaoishi nchi za kigeni pamoja na waturuki wenyewe na utamaduni wao. Huwaunga mkono na kuwasaidia nyakati za shida na furaha. Hurusha matangazo hewani masaa 24 kwa siku kupitia nyuzi za usambazaji, satelite na mtandao. Sikiliza Voice of Turkey (Sauti ya Uturuki) popote ulipo.

 

TRT Kurdish Channel, ni idhaa ya TRT inayowajumuisha wasikilizaji wa umri wowote kwa lengo la kuimarisha umoja na upendo katika nchi yetu. Tangu kuanza matangazo yake tarehe 1 Mei mwaka 2009, imeweza, TRT 6 imeweza kufika kusinimashariki mwa mkoa wa Anatolia. Inadumisha umoja kati ya wananchi wa mkoani na serikali na inatengeza uhusiano mzuri wa Uturuki wa kimataifa.

 

TRT Avrupa FM, idhaa ya sauti nyengine kutoka Anatolia. TRT Avrupa FM inaleta faraja katika maisha, matukio mbalimbali, maadili ya utamaduni wa Kituruki pamoja na miziki mbali mbali. Burudani ya muziki na mazungumzo yanapatikana katika TRT Avrupa FM kwa wale vijana wanaopenda. TRT Avrupa FM hurusha matangazo hewani kila siku kati ya saa 9.00 – 18.00 kwa nyakati za kituruki kupitia nyuzi za usambazaji, satelite na nyaya. Iwapo unataka kusikiliza muziki unaoupenda au kumchezea unayempenda nyimbo au kutuma maoni yako, bonyeza kiunganishi cha TRT Avrupa FM kifuatacho,

http://www.trt.net.tr/Radyo/RadyoAnasayfa.aspx