TRT Historia

TRT-Matukio

Mei 1 1964

Makala ya 359 ilipoanza kutumika katika katiba ya serikali ya Uturuki,Shirika la utangazaji la redio na televisheni(iliitwa TRT tangu hapo na kuendelea) lilianzishwa na kupewa mamlaka kamili kurusha matangazo katika idhaa za serikali.

 

Januari 31 1968

Televisheni ya TRT Ankara ilianza na kufanya majaribio ya kwanza

 

Septemba 9, 1974

Redio ya Uturuki ilianza kutoa matangazo kwa masa 24, na kupewa jina la TRT-1

 

April 17, 1979

TRT iliandaa sherehe za kwanza za “siku ya watoto ya kimataifa” Aprili 23. Tukio hilo lilitangazwa katika idhaa/ vituo 27 barani Ulaya.

 

Oktoba 6, 1986

Idhaa ya televisheni ya TRT-2 ilianzishwa

 

Oktoba 2, 1989

Idhaa za TRT-3 na TRT-gap zilianzishwa kwa wakati mmoja

 

Februari 28, 1990

Idhaa ya kimataifa ya TRT-INT ilianza kutangaza barani Ulaya

 

Julai 30, 1990

Idhaa ya matangazo ya elimu TRT-4 ilianza kurusha matangazo toka Izmir

 

Disemba 3, 1990

TRT ilianzisha majaribio ya teletext kwa kuipa jina “Telegun”

 

Aprili 27, 1992

Idhaa ya TRT Eurasia ilianza kutoa matangazo, ikiwatangazia Waturuki kama wasikilizaji wakuu

 

Novemba 14, 1998

Ofisi ya TRT ilianzishwa mjini Berlin

 

Januari 5, 1999

Kituo kikuu cha teknolojia ya utangazaji wa kidigitali(SAYTEK) kilianzishwa.

 

Mei 1, 1999

Tovuti ya TRT ilianzishwa

 

June 15, 1999

Matangazo ya TRT-FM na Sauti ya Uturuki yalifika Urusi

 

Julai 25, 1999

Matangazo ya TRT-INT TV yalifika Australia na New zealand

 

Septemba 20, 1999

Ofisi ya TRT Ashghabat ilianzishwa huko Turkmenistan

 

Disemba 6, 1999

Redio-4 ilianza kurusha matangazo

 

 

Juni 7, 2000

Matangazo ya TRT-INT, Sauti ya Uturuki(TSR), na TRT-FM(redio-2) yanafika Marekani na Kanada

 

Januari 31, 2001

Idhaa za TRT-TV zilifanywa upya na utambulisho mpya wa Taasisi na nembo mpya

 

Juni 2, 2001

Ofisi ya TRT Baku ilianzishwa

 

Juni 16, 2001

Ofisi ya TRT Cairo ilianzishwa

 

Juni 1, 2002

Kupitia matangazo ya moja kwa moja,  TRT ilitangaza kombe la Dunia la FIFA 2002 ambalo liliandaliwa na nchi za Korea Kusini na Japan katika miji ya Seoul na Tokyo, ambapo timu ya taifa ya Uturuki ilishika nafasi ya tatu.

 

Juni 25, 2002

Ofisi ya tano ya TRT nje ya nchi ilifunguliwa Brus

 

Julai 2, 2002

Redio ya Utalii ya TRT ilianza kurusha matangazo yake masa 24, ikijikita katika kituo cha Lara, na Idhaa ya Antalya ilianza kuwatangazia wasikilizaji wake kwa Kingereza, Kifaransa, Kijerumani, Kirusi na Kigiriki.

 

Agusti 8, 2002

Ofisi ya sita ya TRT nje ya nchi ilifunguliwa Washington DC

 

Mei 24, 2003

Ikiiwakilisha Uturuki katika mashindano ya 48 ya wimbo wa Eurovision, TRT ilishinda nafasi ya kwanza na wimbo wa “Every way that I can” ulioimbwa na Sertab Erener.

 

Januari 20, 2004

Matangazo ya kidigitali ya TRT yalianzishwa. Idhaa za TRT-1, TRT-2, TRT-3, TRT-4, TRT-INT na matangazo ya TRT redio matangazo yak esasa yapo kwa njia ya digitali kupitia satelaiti ya 1C.

 

Mei 12, 2004

TRT iliandaa mashindano ya 49 ya wimbo wa Eurovision. Mashindano yalirushwa katika hatua mbili kwa mara ya kwanza. Matangazo yalirushwa moja kwa moja kwa nchi 36 duniani.

 

Novemba 3, 2004

Tovuti ya TRT www.trt.net.tr ilitengenezwa tena  na mifumo yake kuwekwa kisasa zaidi. Katika hilo; fahirisi yake iliongezwa vitu; muundo wake uliboreshwa ili kuweza kuendana na vivinjari vya mtandao; urambazaji ulifanywa rahisi; tovuti iliongezeka mwendo na ya kueleweka. Mipango ya televisheni, redio na muda iliingizwa kwa kutumianjia mpya zilizowekwa ili watumiaji waweze kupata habari kuhusiana na programu.

 

Disemba 14, 2004

Matangazo ya TV ya TRT-TURK na TSR redio ya Uturuki yalianzishwa kwa kutumia Boriti ya Mashariki ya Satelaiti ya 1C ya Turksat ambayo inajumuisha Uturuki na Asia ya kati.

 

Juni 24, 2005

Ofisi ya saba ya nje ya nchi ilifunguliwa Tashkent

 

Agusti 10, 2005

Matangazo ya ndani na kimataifa yalitangazwa kwa mafanikio mjini  Izmir 2005.

 

November 1, 2005

Umoja wa matangazo wa Trt- Pacific and Asia (ABU). Makunaliano yalitiwa saini.

 

Juni 22 2006,

Kufuatia makubaliano na televisheni ya Buena Vista. Televisheni ikanunua haki ya matangazo kutoka kwa Wall Disney co. Kwa ajili ya katuni, animesheni na filamu kwa miaka minne.

 

Machi 16, 2007

TRT ilinunua haki ya kutangaza kombe la dunia na mashindano mbalimbali ya FIFA kama vile kombe la confederation tangu 2010-2014.

 

Aprili 13-20, 2008

TRT ilinunua haki ya kutangaza matembezi ya kimataifa ya 44 ya baiskeli nchini Uturuki