TRT Habari

TRT HABARI

Malengo.

Malengo ya TRT Habari ni kutangaza habari za kutosheleza na kuaminika kila wakati. TRT habari inakuletea habari kutoka Uturuki na dunia nzima kutoka nyanja ya Uchumi, Sayansi, Teknolojia, Sanaa na utamaduni. Kwa kuambatana na Sheria na uhuru wa demokrasia TRT Habari inatangaza habari ya kuaminika ili kuchangia katika kuimarika kwa demokrasia na kukua kwa fikra huru.

TRT habari inasaidia katika kueneza ukweli wa mada tata zinazokumba ulimwengu kwa kutangaza pande tofauti za mada tata na kwa kuhimiza kuwepo kwa majadiliano.

Kanuni

Kutangaza habari ya kuaminika punde inapotokea. Kuwahusisha wataalamu katika mijadala juu ya mada tata zinazoikabili Uturuki au Dunia. Kuhakikisha ya kwamba fursa ya kutosha imetolewa ya kutoa maoni juu ya mada zinazozikumba nchi au Dunia ili kuhamasisha taswira ya Uturuki kama nchi yenye uhuru wa demokrasia, isiyokuwa na ubaguzi na yenye kuheshimu sheria.  Kupeperusha matangazo kuhusu Uturuki na Dunia nzima bila ubaguzi. Kuleta matangazo kwa upana huku ikiepukana na matangazo yanayoweza kuleta mgogoro katika jamii.

Kutayarisha matangazo ya TV na Redio kwa kufatia sheria kulingana na katiba na kwa kuzingatia kanuni za utangazaji za kutopendelea, usahihi na kutoa habari mara tu zinapotendeka.

Kutayarisha matangazo yanayohusiana na maamuzi, hatua na vitendo vya serikali na kupeperusha makadirio iliyofanywa na wataalamu huru kuhusiana na maamuzi hatua na vitendo vya serikali.

Kuimarisha uhusiano baina ya TRT na vyombo vya habari kutoka nchi za nje na pia kuhakikisha uwiano katika habari zinazopeperushwa kwa mataifa ya nje. Kutangaza habari sio tu kama ilivyotufikia kutoka kwa mashirika ya habari bali baada ya tathmini ya habari hio kulingana na kanuni za sasa za utangazaji.

Kupeperusha habari ya nchi au dunia bila mapendeleo huku tukijali maslahi ya mwananchi wa sasa na jamii ya sasa.

Kutumia teknolojia ya kisasa katika njia mwafaka katika kutayarisha habari na kuipa uzito habari ya moja kwa moja ikilinganishwa na ile iliyorekodiwa. Ishara ya “imerekodiwa” itatumiwa katika matangazo ambayo yamehifadhiwa. Kutumia teknolojia ya kisasa kama vile 3D, grafiki na mifano kwa michoro katika matangazo. Kuepuka mambo yatakayoficha mada muhimu iliyonuiwa kutangazwa.

Kuepuka matangazo yanayoweza kuleta mzozo baina ya nchi na kuhakikisha kuwa chanzo cha habari kimetajwa.

Kupeperusha matangazo yanayohusiana na mada katika nchi kama vile sherehe na maadhimisho kwa njia itakayomvutia mtazamaji bila ya kukiuka sheria na kanuni za utangazaji.

Kuzingatia kwa wakati wote kanuni za kutopendelea, usahihi na kutoa habari mara tu zinapotendeka katika habari za kisiasa. Kutobadilisha maana iliyokusudiwa katika taarifa inayotolewa na wanasiasa au vyama vya siasa  katiak matangazo ya televisheni.

Kutofanya matangazo yanayoegemea upande mmoja. Kutoegemea upande wowote iwe katika siasa, imani,vikundi au maoni. Kutoa mtaja yeyote upande wowote kuwa na hatia hadi mahakama itakapo toa hukumu hiyo.

Kuwapa watu katika jamii fursa ya kufikiria kuhusiana na mambo ya serikali, siasa, uchumi na maswala katika jamii na kupeperusha maoni asili ya watu wengine katika jamii kupitia mijadala na shirika la jamii pamoja na mijadala huru yanayowahusisha watazamaji.