Mumiani 40 wagunduliwa nchini Misri

Mumiani 40 kumi kati yao wakiwa watoto wagunduliwa nchini Misri

Mumiani 40 wagunduliwa nchini Misri

Maiti za kale zilizohifadhiwa "Mumiani" 40 zimegunduliwa  Katika makaburi ya kihistoria yaliyopo mji wa Minye nchini Misri.

Waziri wa mambo ya kihistoria wa Misri Halid el-Anani alitoa taarifa za ugunduzi huoa katika mkutano na wanahabari uliofanyika jijini Cairo.

Waziri Halid alisema katika eneo la Tuna Jabal katika mji wa Minye mumiani 40 wamegunduliwa 10 kati yao ikiwa ni  miili ya watoto.

Kati ya mumiani hao wapo ambao walizikwa na masunduku "jeneza", wapo ambao walizikwa bila masunduku "jeneza".

Haikusemwa kwamba mumiani hao ni wa zama zipi.

 


Tagi: Mumiani , Misri

Habari Zinazohusiana