Mashua mbili zazama Mediterania ,wahamiaji 170 waangamia

Wahamiaji zaidi ya 170 waangamia  katika bahari ya Mediterania  baada ya mashua zao kuzama

Mashua mbili zazama  Mediterania ,wahamiaji 170 waangamia

Kulingana na taarifa iliotolewa na  shirika la Umoja wa Mataifa ambalo linahusika na kutoka huduma kwa wakimbizi imesema kuwa watu 53 wamefariki  kutokana na mashua  yao kuzama Alboran kati  ya Morocco na Uhispania.

Taarifa hiyo imethibitishwa pia na mashirika yasiokuwa ya  kiserikali.

Ajali mbili zilizotokea katika bahari ya Mediterania zimesababishwa vifo vya watu  zaidi ya 170 ambao ni wahamiaji waliokuwa katika msafara wao kuelekea barani Ulaya.

Mtu mmoja alieokolewa masaa  24 baada ya tukio hilo anapewa matibabu nchini Morocco.

Kamishna mkuu wa Umoja wa Mataifa Filippo Grandi amesema kuwa  kuendelea kwa maafa ya wahamiaji  ni jambo lisiloridhisha.

Tukio jingine  limetangazwa na jeshi la wanamaji wa Italia imefahamisha kuwa wahamiaji 117 wameangamia  baada ya amshua yao kuzama.Habari Zinazohusiana