Mike Pompeo  awasili nchini Misri katika ziara yake Mashariki ya Kati

Mike Pompeo awasili nchini Misri katika ziara yake rasmi Mashariki ya Kati

Mike Pompeo  awasili nchini Misri katika ziara yake Mashariki ya Kati

kulingana na taarifa zilitolewa na jarida la  la MENA nchini Misri, Mike Pompeo aliwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa mjini  Cairo majira ya usiku Jumatano.

Mike Pompeo amejielekeza nchini Misri baada ya kufanya ziara ya kushtukiza nchi Irak.

Katika ziara yake hiyo nchini Misri , Mike Pompeo anataraj kuzungumza na Samih Shukri. Katika mkutano wao  viongozi hao watajadili kuhusu  ushirikiano kati ya Marekani na Misri na hali inavyoendelea Mashariki ya Kati.

Pompeo katika ziara yake hiyo  ilioanzia nchini Yordai alijielekeza nchini Iraq na kuzungumza na rais Salih, waziri wake mkuu Adil Abdulmehdi na msemaji wa bunge Mohammad  al Halbusi.

Mike Pompeo anatarajiwa  kujielekeza nchini Saudia, Qatar, Falme za kiarabu, Bahrein , Oman  na Kuweit.Habari Zinazohusiana