Omar al Bashir, rais wa Sudan asema jeshi lipo tayari kulinda mali ya umma

Rais wa Sudan Omar al Bashir  asema kuwa  jeshi  lipo tayari kukabiliana na njma za maadui

Omar al Bashir, rais wa Sudan asema jeshi lipo tayari kulinda mali ya umma

 

Rais wa Sudan Omar al Bashir  asema kuwa  jeshi  lipo tayari na lina uwezo wa ulinda mali ya umma.

Omar al Bashir  rais wa Sudan  asema kuwa  jeshi linafaulu kukabiliana na njama za  wahaini na kuendelea kulinda maslahi ya taifa.

Hayo rais wa Sudan ameyazungumza  katika hotuba yake aliotoa katika  hafla maalumu ya jeshi la Sudan iliofanyika  Kaskazini-Mashariki mwa mji wa Atbara.

Ifahamike kuwa  maandamano ya kupinga kupanda kwa bei za bidhaa mahitaji nchini Sudan  yaliiubuka Disemba 19  mini Atbara.

Mjini huo ndio kitovu cha maandamano hayo ya kupinga kupanda kwa bei za  bidhaa mahitaji.

Ofisi za chama tawala nchini Sudan zilichomwa moto  na waandamanaji.

Taarifa rasmi zilizotolewa na uongozi wa Atbara ulifahamisha kuwa ni watu ndio waliofariki katika maandamano.

Katika hotuba yake , rais El Bashir amekemea waliochochce maandamano hayo na kuwataka raia kutokashawishika kwa kuwa walioandaa maandamano hawana nia nzuri na Sudan.

Rais wa Sudan  amepongeza pia jeshi kwa kukabiliana na njama za maadui wa Sudan wanaojaribu kutumia nyoyo za raia  waliodhaifu.

Kwa ujumla watu 19  ndio waliotangazwa kufariki  katika maandamano.Habari Zinazohusiana