Jeshi lakomboa maeneo yaliyokuwa yametawaliwa na Boko Haramu nchini Nigeria

Wanajeshi wameyakomboa maeneo yaliyokuwa yametawaliwa na magaidi wa Boko Haramu nchini Nigeria.

Jeshi lakomboa maeneo yaliyokuwa yametawaliwa na Boko Haramu nchini Nigeria

Wanajeshi wameyakomboa maeneo yaliyokuwa yametawaliwa na magaidi wa Boko Haramu nchini Nigeria.

Kwa mujibu wa habari,maeneo zaidi ya 20 yalikuwa chini ya utawala wa magaidi wa Boko Haramu ndani ya miaka mitatu iliyopita.

Kiongozi wa jimbo la Borno Kashim Shettima, amekumbushia jinsi magaidi wa Boko Haramu walivyofanya mashambulizi ya hali ya juu mwaka 2013-2014 na kuchukua utawala wa maeneo 27.

Kashim Shettima,ameongeza kwa kusema kuwa nguvu  ya kundi la Boko Haramu ilianza kupungua toka mwaka 2015 baada ya jeshi kuanza kufanya mashambulizi dhidi ya magaidi hao.

Kati ya maeneo 27 yaliyochukuliwa na magaidi hao,maeneo 20 yamekombolewa na wananchi kujengewa zaidi ya nyumba elfu thelathini.

Mateka wameachiwa huku baadhi ya magaidi wakiwa wamejisalimisha.Habari Zinazohusiana