Rwanda na mradi kabambe wa teknolojia  barani Afrika "Silicon Valley”

Mradi kabambe wa teknolojia mithili ya ”Silicon Valley” kuanza  katika eneo la hekari 70 mjini Kigali nchini Rwanda

Rwanda na mradi kabambe wa teknolojia  barani Afrika "Silicon Valley”

Mradi kabambe wa teknolojia   ambao utajumuisha makampuni tofauti ya teknolojia  wataraji kuanza  mjini Kigali katika eneo la hekari 70.

Mradi huo utaanikishwa  nchini Rwanda kwa ushirikiano na  jukwaa la  maendeleo  ya miundombinu la benki ya maendeleo ya Afrika .

Jukwaa hilo linafahamika kama  ”Africa 50”.

Mradi huo utatumia kiwango cha dola bilioni 2 huku Benki ya Maendeleo ya Afrika ikifahamisha kwamba itatumia kiwango cha dola milioni 400.

Mradi huo unajumuisha  ujenzi wa vyuo vikuu, vituo vya teknolojia   ya kisasa na vituo vya biashara.

Wanafunzi zaidi ya 2600  kila mwaka watakuwa wakihitimu katika mafunzo ya teknolojia.

Waziri mkuu wa Rwanda Edouard Ngitente amesema kuwa mradi  huo ni miongoni mwa miradi ya ”Vision 2020” ambao ni malengo  ya Rwanda kufikia ifikapo mwaka 2020.Habari Zinazohusiana